Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbeya: Dk Tulia ahamasisha wananchi kulinda kura na kuichagua CCM

Spika wa Bunge na mgombea ubunge wa Jimbo jipya la Uyole, Dk Tulia Ackson (kushoto), akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Busokelo, George Mwalwiba, katika uzinduzi wa kampeni uliofanyika Septemba 6, 2025, Shule ya Lwangwa, Rungwe.

Muktasari:

  • Kauli hiyo ameitoa leo Jumamosi Septemba 6,2025 wakati akizindua  kampeni na kumnadi  mgombea  ubunge jimbo la Busokelo  Wilaya ya Rungwe mkoani hapa, George Mwalwiba.

Mbeya. Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Dk Tulia Ackson amewahimiza wananchi wa Wilaya ya Rungwe kuhakikisha wanalinda kura na kuwachagua wagombea wa CCM katika nafasi za urais, ubunge na udiwani, ili chama hicho kiweze kuunda Serikali na kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo.

Dk Tulia ambaye pia ni mgombea ubunge wa Jimbo jipya la Uyole, ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, Septemba 6, 2025, alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi na kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Busokelo, George Mwalwiba, katika Wilaya ya Rungwe.

Akizungumza katika mkutano huo wa kampeni, Dk Tulia amesema wananchi wa Rungwe wanayo dhamana kubwa ya kuendeleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuichagua CCM katika ngazi zote za uongozi.

“Ni muhimu tukalinda kura zetu na kuhakikisha tunachagua wagombea wa CCM kuanzia urais, ubunge hadi udiwani. Kwa kufanya hivyo, tunatoa nafasi kwa chama chenye dira na ilani yenye majibu ya changamoto za wananchi kuendelea kuongoza nchi,” amesema Dk Tulia.

Aidha, amepongeza maendeleo yaliyofikiwa katika Mkoa wa Mbeya, ikiwemo sekta za elimu, afya, maji na barabara, akisisitiza kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya usimamizi madhubuti wa Serikali ya CCM.

Dk Tulia amewataka wananchi kutofanya maamuzi ya majaribio wakati wa uchaguzi, bali wachague viongozi wenye uwezo wa kutekeleza majukumu kwa ufanisi na kwa kuzingatia maslahi ya Watanzania.

" Ifikapo Oktoba  29, 2025 wananchi mkatie tiki wagombea wa CCM ili kuwawezesha kuunda Serikali ambayo itaenda kukamilisha kazi iliyo anzishwa katika suala zima la kuleta maendeleo  ya kweli," amesema.

Amesema Serikali ya awamu ya sita imeleta maendeleo  na kuboresha huduma katika sekta ya afya, elimu, barabara  na maji hususani  mradi mkubwa  wa kimkakati  wa chanzo  cha maji kutoka  Mto Kiwira  wenye thamani ya zaidi ya Sh119 bilioni.

"Wananchi  wa Busokelo Serikali  ya awamu wa sita imefanya kazi kubwa na nzuri chini ya Rais Samia Suluhu  Hassan hususani sekta mbalimbali za afya ,elimu na miundombinu ya barabara na maji ," amesema.

Dk Tulia amesema kuwa uwekezaji huo unapaswa kuungwa mkono na wananchi kwa kuwapigia kura wagombea wa nafasi mbalimbali kutoka CCM.


Ahadi za mgombea

Akizungumza  na wananachi waliojitokeze  kwenye uzinduzi wa kampeni uliofanyika  katika viwanja vya Shule ya Msingi Lwangwa Halmashauri ya Busokelo, Mwalwiba  ameomba ushirikiano na wananchi ili aweze kuboresha miradi  mbalimbali ya maendeleo.

"Kwanza nashukuru sana kwa wananchi  kwa kuniamini sambamba na Chama cha Mapinduzi, nitakwenda kutekeleza  ilani ya uchaguzi  kwa vitendo katika kuleta maendeleo  kwenye nyanja  mbalimbali za kiuchumi  ikiwepo elimu,afya na nyinginezo," amesema.

Mkazi wa Kandete, Frank  Daudi amesema kimsingi wana imani na mgombea ubunge jimbo la Busokelo  kikubwa wanahitaji maendeleo  ya kweli katika nyanja mbalimbali  katika  kuunga mkono  juhudi  za Serikali ya awamu ya sita.