Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ulega: Tanzania inahitaji mitaji, teknolojia kuvutia vijana

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega

Muktasari:

  • Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Tanzania inahitaji mitaji na teknolojia ya kisasa ili iweze kuvuta kinamama na vijana zaidi katika sekta hiyo.

Dar es Salaam. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Tanzania inahitaji mitaji na teknolojia ya kisasa ili iweze kuvuta kinamama na vijana zaidi katika sekta hiyo.

Ameyasema hayo wakati akizungumza katika Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika 2023 (AGRF), ulioanza leo Septemba 5 hadi 8 jijini hapa.

"Shida yetu kubwa ni mitaji teknolojia na masoko, hata upande wetu wa mifugo na uvuvi ni mambo tuliyoyapa kipaumbele tutayaonyesha kwa waliotayari kuwekeza ili waweze kupata faida kwa haraka," amesema Ulega.

"Tunahitaji teknolojia ya kisasa ili iweze kuvuta kinamama na vijana ambao ndiyo asilimia kubwa ya watu tulionao na watu tunaowahitaji kufanya shughuli hizi," amesema Ulega.

Amesema kama wizara ya mifugo imejipanga kuiambia dunia kuwa wanahitaji kuzalisha mayai mengi ya kula ndani ya nchi na kuuza nje.

"Nchi zenye matatizo makubwa kama Somalia, tumeona tumekuwa tukipeleka vyakula kama mahindi yanayopelekwa kwa kiasi kikubwa na yananunuliwa na mashirika ya kimataifa kama Shirika la Chakula Duniani (WFP), lakini kwa shida iliyopo tunaweza kuwapelekea na vyakula vya protini," amesema Ulega.

Amesema vyakula hivyo vinaweza kuwa mayai fursa anayoiona kwa ukubwa huku akieleza kuwa matamanio yake ni kuona siku moja Watanzania wanafanya uwekezaji kwa kutengeneza mayai ikiwezekana yaliyochemshwa kufungashwa kabla ya kupelekwa kwa wahitaji.

"Tuone malori yanatoka na kwenda nchi za kaskazini,"

Kuhusu malisho ya mifugo alisema nayo ni fursa inayoweza kutazamwa kibiashara kwa ajili ya mifugo ya ndani na kuuzia wengine ambao hawajapata mvua kwa miaka mingi.

"Mifugo imekuwa imekuwa ikihangaika kwa kiasi kikubwa sana hasa katika upande wa malisho, tuanze kuyatazama majani kwa ajili ya biashara na hii inaweza kusaidia kuondoa migogoro ya wafugaji na wakulima," amesema Ulega.