Mahakama yabadili gia kesi ya Lissu

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeridhia ombi la upande wa mashtaka la kutaka kesi ya kuchapisha taarifa za uongo inamkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu kusikilizwa kwa njia ya mtandao na badala yake imekubalia na upande wa utetezi wa kutaka mshtakiwa huyo amepelekwa mahakama kusikiliza kesi yake.
Uamuzi huo umetolewa leo Jumanne, Mei 6, 2025 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Geoffrey Mhini, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa kutolewa uamuzi.
"Kwa misingi ya utoaji haki, naelekeza mshtakiwa huyu tarehe ijayo aletwe Mahakama ya Kisutu ili aweze kusikiliza kesi yake kwa njia ya kawaida," amesema hakimu Mhini wakati akitoa uamuzi.
Endelea kutufuatilia Mwananchi na Mitandao yetu.