Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lissu, Jamhuri mshikemshike tena leo mahakamani

Muktasari:

  • Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Tundu Lissu anakabiliwa na kesi mbili mahakamani ya uhai na kuchapisha taarifa za uongo mitandaoni.

Dar es Salaam. Kesi mbili za jinai zinazomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu (57), leo Jumane, Mei 6, 2025 tena zinatarajiwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Dar es Salaam inayoketi Kisutu, katika hatua tofautitofauti.

Lissu anakabiliwa na kesi mbili tofauti za jinai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Dar es Salaam, Kisutu, moja akikabiliwa na shtaka moja la uhai na nyingine akikabiliwa na mashtaka matatu ya kuchapisha taarifa za uwongo mitandaoni.

Alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza na kusomewa mashtaka hayo, Aprili 10, 2025. Kesi hizo zote zimepangwa kuendelea leo katika hatua tofautitofauti.

Wakati kesi ya uhaini imepangwa kwa ajili ya kutajwa kuangalia maendeleo ya upelelezi, kama umeshakamilika ili kuendelea na hatua zinazofuata, kesi ya mashtaka ya kuchapisha taarifa za uongo mitandaoni imepangwa kwa ajili ya uamuzi wa namna ya uendeshwaji wake.

Hoja kubwa inayobishaniwa na ambayo inatarajiwa kuamuriwa leo katika kesi hiyo ni iwapo kesi hiyo pia iendeshwe kwa njia ya mtandao, au la.

Usikilizwaji wa kesi kwa njia ya mtandani ni utaratibu wa uendeshaji wa kesi huku mshtakiwa na au wahusika wa upando mmoja au pande zote za kesi wakiwasiliana kwa picha jongefu (video conference) kutokea maeneo mengine bila kufika mahakamani.

Uamuzi huo wa njia au njia gani itumike kuendesha kesi hiyo unatokana na mvutano ulioibuka baina ya upande wa mashtaka na mahakama kwa upande mmoja na mshtakiwa na mawakili wake kwa upande mmoja, wakati kesi hizo zilipoitwa Aprili 24, 2024.

Siku hiyo mshtakiwa hakufikishwa mahakamani badala yake mahakama ilikuwa imeandaa utaratibu wa kuzisikiliza kwa njia hiyo mtandao, huku jeshi la Polisi likizuia watu wote waliotaka kuingia mahakamani kufuatilia kesi hiyo wakiwemo wanahabari.

Kesi ya kwanza kuitwa ilikuwa ni kesi kuchapisha taarifa za uwongo mtandaoni, ambayo ilikuwa imepangwa kwa ajili ya usikilizwaji wa wali (mshtakiwa kusomewa muhtasari wa kesi.

Hata hivyo, kesi hiyo haikuweza kuendelea baada ya Lissu kugoma kujiunga mtandaoni akiwa katika mahabusu ya gereza la Ukonga, kupinga kesi yake kuendeshw akwa utaratibu huo, akitaka afikishwe mahakamani.

Mawakili wake waliokuwa mahakamani hapo katika kituo cha kuendesha kesi kwa mtandao waliwasilisha hoja kupinga utartibu huo wakidai kuwa ni kinyume na matakwa ya sheria ambayo inataka kesi za jiani kuendeshwa katika mahakama ya wazi.

Walisisitiza ingawa kuna Kanuni za Uendeshaji Mashauri kwa njia hiyo, lakini kanuni hizo zina utaratibu wake ambao pia haukuwa umefuatwa huku wakihoji ni nani aliyeamua utaratibu huo bila hata kumshiriikisha mshtakiwa.

Vilevile walidai kuwa katika hatua hiyo sheria inelekeza kuwa mshtakiwa anapaswa kuwepo mahakamani kwa ajili ya kusaini hoja zitakazoainishwa kama hoja zinazobishaniwa kabla ya mahakama kuanza kupokea ushahidi.

Pia mawakili hao walilalamika mteja wao kutokutendewa haki mahabusu ikiwa ni pamoja na wao kunyimwa fursa ya kuonana na kushauriana na mteja wao mahabusu, haki ya kuabudu pamoja na wanananchi na wanahabari kuzuiwa kuingia mahakamani kufuatilia kesi hiyo.

Hivyo walitaka Mkuu wa Magereza ya mkoa wa Dar es Salaam kuitwa mahakamani kujieleza pamoja na Jeshi la Polisi kwa ukiukwaji huo wa haki za mteja wao na za wananchi kwa ujumla.

Katika kesi ya uhaini pia mawakili wa pande zote walivutana kwa hoja kuhusu kesi huyo kuendeshwa kwa utaratibu huo, lakini Hakimu Mkazi Mkuu, Mfawidhi, Francio Kiswaga alitoa uamuzi wake siku hiyo hiyo.

Katika uamuzi huo pamoja na maelezo mengine alieleza kuwa Mahakama kwa mujibu wa kanuni hizo ina mamlaka ya kuamuru kesi kuendeshwa kwa mtandao, hivyo akamua kuwa kesi hiyo itaendeshwa kwa utaratibu huo.

Kesi hiyo ambayo upelelezi wake ulikuwa bado haujakamilika, iliahirishwa mpaka kesho kwa ajili ya kutajwa kuona hali ya upelelezi.

Hata hivyo jopo la mawakili wa Lissu linaloongozwa na mawakili Mpale Mpoki, Dk Rugemeleza Nshala, Peter Kibatala na wengine walieleza kuwa hawajaridhishwa na uamuzi huo na kwamba watajadiliana na mteja wao kuona hatua zaidi za kuchukua.

Hata hivyo walibainisha kuwa mteja wake ameshaweka msimamo kuwa hayuko tayari kushiriki kesi hizo kwa utaratibu huo badala ya kufikishwa mahakamani.

Aprili 28, 2025 upande wa mashtaka ulijibu hoja hizo ulipnga hoja za upande wa utetezi ukidai kuwa utaratibu huo ni sahihi na kwamba kesi kuendeshwa kwa utaratibu huo haina maana kwamba si mahakama ya wazi.

Walisisitiza kuwa si mara ya kwanza kesi kuendeshwa kwa utaratibu huo, huku wakidai kuwa katika magereza wana taratibu zao ambazo zinapaswa kufuatwa na watu wote wakiwemo wafungwa na mahabusu na kwmaba hivyo hawaoni sababu ya kuwaita maafisa wa majeshi hayo kujieleza.

Mahakama baada ya kusikiliza za pande zote, Hakimu Godfrey Mhini anayesikiliza kesi hiyo aliahirisha kesi hiyo pia mpaka leo kwa ajili ya uamuzi kama kesi hiyo iendelee kusikilizwa kwa mtandao au mahakama itoe amri mshtakiwa afikishwe mahakamani.

Hata hivyo, Jumamosi ya Mei 3, 2025 mawakili wa Lissu walifanya mkutano na waandishi wa habari wakifafanua kwa kina ukiukwaji huo wa haki za mteja wao mahabusu na namna hata wao wanavyopata tatu kuona na kujadiliana na mteja wao huo mahabusu.

Pia walielezea kutokuridhishwa na kitendo cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, kuzungumzia bungeni kesi hiyo huku akitetea utaratibu wa kesi hiyo kuendeshwa kwa mtandao kuwa ni sahihi na kupinga madai mbalimbali yaliyotolewa na mawakili wa Lissu.

Mbali na Johari pia walieleza kusikitishwa na kauli za Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa ambaye alituzungumzia sababu za Mahakama kuendesha kesi hiyo kwa njia ya mtandao, hoja ambazo ndizo zilikuwa zinasubiriwa kuamuriwa.

Walikemea kauli hizo wakidai hayo waliyoyafanya ni kuingilia uhuru wa mahakama katika uamuzi ambao unasubiriwa kutolewa kuhusiana na suala hilo.

Hata hivyo jana Jumatatu, Mei 5, 2025 Wakili Peter Kibatala alilieleza Mwananchi baada ya mkutano huo wanahabari alipokwenda kuonana na mteja wake huyo alibaini mambo yalikuwa yamebadilika kwani hakupata usumbufu kama ilivyokuwa awali bali alihudumiwa vema.

Ingawa katika mkutano wao na wanahabari mawakili hao walisema kuwa mteja wao alikuwa amepanga kuanza mgomo wa kutokula huko mahabusu kupinga pamoja na mambo mengine, kukiukwa haki zake, lakini jana wakili Kibatala alilieleza Mwananchi kuwa bado hajaanza mgomo huo.

“Bado hajanza mgomo lakini siwezi kukueleza hapa hewani (kwenye simu) kwa undani ila kuna mambo mengine tutazungumza vizuri zaidi kesho (leo) mahakamani,” amesema Kibatala.