Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Ulega: ‘Gesti’ za mifugo mbioni kuanzishwa nchini

Muktasari:

  • Katika mpango huo, Serikali itajenga miundombinu mizuri ikiwemo majosho na mabwawa ya kunyweshea mifugo ili kuwawezesha wafugaji kufanya shughuli zao za unenepeshaji wa mifugo na kuivuna katika mazingira bora na hivyo kukuza kipato chao.

Dodoma. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, amesema Serikali imejipanga kuanzisha gesti za mifugo (livestock guest house), katika Ranchi za Taifa (NARCO), ili kuwapa fursa vijana na wafugaji kuiweka mifugo yao ili kuiongezea thamani.

Waziri Ulega ameyasema hayo wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya hali ya sekta ya mifugo nchini, kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, kilichofanyika jijini Dodoma leo Agosti 24, 2023.

Kwa mujibu wa waziri huyo, wafugaji wataruhusiwa kuingiza mifugo katika ‘gesti’ kwa kipindi cha muda maalum, na kisha kuwaingiza katika masoko ya ndani na nje ya nchi na hivyo kujipatia bei nzuri, ambayo itawainua kiuchumi.

Alisema Serikali ipo katika mpango wa kuweka miundombinu mizuri ikiwemo majosho na mabwawa ya kunyweshea mifugo itakayowawezesha wafugaji kufanya shughuli zao za unenepeshaji wa mifugo na kuivuna ili kukuza kipato chao.

Aliongeza kuwa wataweka utaratibu mzuri wa kuwapata vijana na wafugaji wengine ambao watakuwa tayari kupeleka mifugo yao katika gesti hizo lengo likiwa kuwafanya wafugaji waone tija ya ufugaji wa kisasa, na hivyo kuondokana na ufugaji wa kuhamahama, ambao umekuwa ukiwaingiza matatizoni kila uchao.

Wazir Uledi amfafanua kuwa kwa kuanza, wataweka miundombinu hiyo katika Ranchi ya Mkata iliyopo mkoani Morogoro, ili kuwapa nafasi wafugaji waliopo katika Bonde la Mto Kilombero waweze kufanya ufugaji wao humo na kuondokana na ufugaji holela.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kama hiyo, David Kihenzile, amepongeza juu ya mpango huo akisema: “Huu ni mpango mzuri sana, wizara ifanye haraka kutekeleza kwa gharama nafuu na pia kuona umuhimu wa kuueneza nchi nzima ili vijana na wafugaji wengine waweze kunufaika nao.”