Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge CCM aipinga bajeti ya ujenzi, awaita mawaziri waongo

Mbunge wa Sumve (CCM), Kasalali Mageni

Muktasari:

  • Mageni amesema hawezi kuunga mkono bajeti ya Wizara ya Ujenzi badala yake anataka watu wagawane mbao ili kila mtu atoke na chake.

Dodoma. Mbunge wa Sumve (CCM), Kasalali Mageni leo Jumanne Mei 6, 2025 amekuwa mbunge wa kwanza kusikika akipinga bajeti ya Serikali kwa madai ya kuchoshwa na uongo.

Mageni ameipinga bajeti ya Wizara ya Ujenzi iliyowasilishwa jana Jumatatu, Mei 5, 2025 na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ambaye aliomba Bunge limpitishie Sh2.28 trilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo na matumizi mengine.

Kauli ya Mageni inakuwa ya kwanza kusikika tangu mkutano wa 19 katika Bunge la 12 maalumu la kujadili bajeti za Serikali jijini Dodoma tangu ulipoanza Aprili 8, 2025 ambapo wabunge wamekuwa wakiunga mkono tangu kuanzia hotuba ya Waziri Mkuu na zilizofuata.

Amewataja marais watatu, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete, John Magufuli ambao kwa nyakati tofauti walipofika wilayani humo, Mkoa wa Mwanza waliahidi ujenzi wa barabara lakini hilo halikufanyika na wilaya hiyo imeendelea kutounganishwa kwa lami.

“Mwaka 1995 Rais Mkapa akiwa anaomba kura aliahidi atatuunga na haikufanyika, mwaka 2005 wakati Kikwete anaomba kura alituahidi na haikufanyika, mwaka 2015 Magufuli wakati akiomba alituahidi na haikufanyika.

“Mwaka 2022 kwa sababu tuna uhaba wa ziara za viongozi wa kitaifa wakifika Mkoa wa Mwanza wanakwamishwa kwenda Kwimba kwa sababu hakuna barabara zinazoeleweka, Makamu wa Rais alipita akaelekeza wizara muende mkaone mtengeneze hamkwenda, nafikiri sisi Mkoa wa Mwanza tuliwekwa kimakosa, haiwezekani sisi pekee hatujaunganishwa,” amesema.

Amesema ukiangalia historia ya Wilaya ya Kwimba ni kongwe, lakini Wilaya ya  Maswa, Geita, Bukoba, Shinyanga na Mwanza yenyewe kuna lami kasoro wao: “Sasa leo nimetumwa kuja kugawana mbao humu.”

Mbunge huyo amesema Waziri Ulega ameingia kwenye mtego wa kudanganya kama ilivyokuwa watangulizi wake akiwataja Dk Leonard Chamulilo, Profesa Makame Mbarawa na Innocent Bashungwa.

“Haiwezekani tuwe tunakufuata fuata, mheshimiwa Waziri (Ulega) wizara yako imeshiriki uongo sana si wewe, ameanza Mzee Chamulilo ameshiriki uongo, akaja Mbarawa akashiriki uongo, akaja Bashungwa akashiriki uongo na wewe una kilomita kumi feki,” amesema.

“Siungi mkono bajeti yako kama ni mbao basi tugawane hapahapa nasi tumechoka kudanganywa, mnatupa barabara hewa kila wakati lakini hakuna kinachoendelea,” amesema.

“…kama siwezi kuwapiga mkaumia bora nioneshe nimekasirika, hizi ni hasira za watu wa Sumve wamenituma kuja kuziwasilisha

Kwa mujibu wa mbunge huyo, jumla ya kilomita 73 za barabara ya eneo hilo zimekuwa zikitajwa kwenye makaratasi ambayo hata magari hayawezi kutembea juu yake.

Mageni ameliambia Bunge jimbo lake la Sumve linatoka kwenye Wilaya kongwe nchini (Kwimba) ambayo imezaa wilaya zaidi ya tatu lakini zote zilizozaliwa huko zimekuwa na lami isipokuwa anakotoka.

Akijibu hoja hiyo, Waziri Ulega amesema: “Mtani wangu usiwe na wasiwasi, nimekusikia na jambo lipo katika vitabu. Nataka nikuhakikishe nina safari ya Mwanza, nitakwenda hadi Sumve na ninajua sasa hivi watani mnapenda sana maendeleo na mimi nataka usikasirike na hutaharibikiwa kwa sababu ya barabara.”

Ulega amesisitiza:“Watu wa kule Sumve kama tatizo ni hili tutajitahidi kwenda kukutetea labda kuwe na tatizo jingine.”