Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chadema watangaza maandamano kudai umeme, maji Dar

Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Kibamba Earnest Mgawe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto ya maji na umeme.

Muktasari:

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Kibamba kimepanga kufanya maandamano ili kujua tatizo la maji na umeme Jimbo la Kibamba, jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Kufuatia kuwapo kwa mgawo wa maji na umeme katika Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeandaa maandamano ya amani kwenda ofisi hizo ili kujua kiini cha tatizo.

  

Maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika Jumatatu Novemba 28, 2022 na Jumanne yanatarajia kuhusisha wananchi, kwenda kwenye ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) Wilaya ya Ubungo.


Hivi karibuni Tanesco ilieleza inakabiliwa na upungufu wa umeme megawati 300-350 kwa siku hali inayosababisha taasisi hiyo kushindwa kuhudumia wateja wake wote kama ilivyokuwa hapo awali.


Kutokana na upungufu huo unaotarajiwa kudumu hadi Januari 2023, ili mifumo yake iendelee kuwa imara nakuleta ufanisi unaotakiwa  inalazimika baadhi ya maeneo nchini kukosa  huduma hiyo kwa mgao ambao utakuwa unadumu masaa manane hadi 12.

Leo Ijumaa, Novemba 25, 2022 Mwenyekiti wa Jimbo la Kibamba wa Chadema, Ernest Mgawe akizungumza na waandishi wa habari amesema changamoto ya umeme inaafanya maisha ya wananchi kuwa magumu.


"Watu wengi wanategemea umeme kuendesha maisha yao, wapo wanaouza vinywaji baridi na wengine wenye saluni kitendo cha kujatika umeme siku nzima kinawaathiri," amesema Mgawe.


Amesema wafanyabiashara wamekuwa wakiteseka kutokana na kutofanya biashara, mtu ana majukumu lakini anapoamka asubuhi kwenda kazini anakaa hadi jioni bila kufanya chochote wakati huo familia inategemea.


 "Wapo wajasiriamali wanaoendesha maisha yao na familia zao kwa kuuzaa vinywaji baridi, kutokuwa na umeme tunarudishana nyuma kimaendeleo mamlaka zinapaswa kujitathimini," amesema.


Kuhusu suala la maji, Mgawe amependekeza mradi wa maji wa Kigamboni uliozinduliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassa, usambazwe kwenye maeneo yenye changamoto.


Alipotafutwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii wa Dawasa, Nelly Msuya amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amefanya ziara kwenye vyanzo vya maji na kutoa maelekezo.


Katika ziara hiyo Makalla ametangaza kutokuwa na mgawo wa maji ndani ya mkoa huo na kuitaka Dawasa kuelekeza nguvu zake kuimarisha miundombinu na miradi mikubwa ikiwemo Mabwepande.


Oktoba 24 mwaka huu, Makalla alitangaza kuwepo kwa mgawo wa majibu baada ya kutembelea vyanzo vya kuzalisha maji vya Ruvu Chini na Ruvu Juu na kujionea upungufu katika uzalishaji wa maji kulikosababishwa na ukame.