Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mwinyi ateua majaji wanne, yumo Raya

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi

Muktasari:

  • Baada ya uteuzi huo, Mahakama Kuu ya Zanzibar imefikisha Majaji wa Mahakama Kuu 18

Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amewateua majaji wanne wa Mahakama Kuu Zanzibar akiwemo Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Raya Issa Msellem.

Pia amemteua Dk Mahadhi Juma Maalim kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Mansura Mosi Kassim, uteuzi huo umeanza leo Julai 15, 2026.

Taarifa hiyo imewataja majaji wengine walioteuliwa ni Valentine Andrew Katema ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa mrajisi wa Mahakama Kuu Zanzibar.

Mwingine ni Khamis Ali Simai ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Hakimu wa Mkoa.

Baada ya uteuzi huo, Mahakama Kuu ya Zanzibar imefikisha majaji 18.