Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Brenda Msangi asisitiza umuhimu wa wazazi kuwekeza kwa watoto wa kike

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi akizungumza katika Jukwaa la nne la The Citizen Rising Woman lililofanyika Machi 8, 2024 katika ukumbi wa Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam leo.

Muktasari:

  • Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Brenda Msangi amesema uwekezaji kwa mtoto wa kike unapaswa kuanza katika ngazi ya familia.

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Brenda Msangi amesema kuna haja kubwa ya wazazi kufanya uwekezaji kwa watoto wa kike kwa kuwa wanaweza kufanya makubwa.

Brenda amesema hayo leo Machi 8, 2024 wakati akiongoza hafla ya The Citizen Rising Woman iliyoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL).

Akizungumzia kauli mbiu ya, “Count her in,” Brenda amesema uwekezaji kwa mtoto wa kike unapaswa kuanza katika ngazi ya familia, hivyo kuwataka wazazi kuona umuhimu wa kufanya uwekezaji huo.

Akitolea mfano wake, amesema wazazi wake walifanya uwekezaji mkubwa kwao akiwamo yeye na dada yake ambaye kwa sasa wote ni wakurugenzi.

“Count her in,  kwangu mimi inaanza kwenye ngazi ya familia, hii inaonesha kuna umuhimu wa kuwekeza kwa watoto wa kike, sisi ni mfano kwamba wazazi wakiwekeza kwa mtoto wa kike wanaweza kufanya makubwa.

“Niwapongeze MCL mnastahili pongezi kwa kuendelea kuwa mfano wa kupeperusha bendera inayoheshimisha wanawake,” amesema Brenda.

Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa, katika kipindi cha miaka minne ya Jukwaa la Rising Woman amekuwa akishiriki kusherehekea mafanikio ya wanawake akiwa miongoni mwa wanawake 217 ambao hadithi zao zimechapishwa.