LIVE: Rais Samia akishiriki kampeni ya ‘The Citizen Rising Woman’

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tuzo za msimu wa nne wa kampeni ya ‘The Citizen Rising Woman’ zinazofanyika leo Machi 8, 2024 katika ukumbi wa The Super Dome uliopo eneo la Masaki, jijini Dar es Salaam.
Rais Samia pia anatarajiwa kushiriki mahojiano ya ana kwa ana kuhusu mchango wa Serikali katika kuwezesha wanawake nchini kwenye uongozi wa nyanja mbalimbali.
Itakumbukwa tuzo hizi zilianza kuratibiwa na Kampuni ya MCL mwaka 2021.
Endelea kufuatilia Mwananchi na mitandao yake.