Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mususa: Ni wakati mwafaka wa kutathimini safari ya usawa kijinsia

Mwenyekiti wa Bodi ya Mwananchi Communication Ltd, Leonard Mususa akizungumza katika Jukwaa la nne la The Citizen Rising Woman lililofanyika Machi 8, 2024 katika ukumbi wa Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam leo.

Muktasari:

  • Wakati dunia ikiadhimisha siku ya mwanamke, Mwenyekiti ya Bodi ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Leonard Mususa amesema ni wakati muafaka wa kutathmini usawa wa kijinsia.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Leonard Mususa amesema amesema katika Siku ya Wanawake Duniani ni wakati muafaka wa kufanya tathmini ya ajenda ya safari ya nchi kuelekea usawa wa kijinsia katika nyanja mbalimbali.

Mususa ametoa kauli hiyo leo katika jukwaa la nne la The Citizen Rising Woman lililofanyika jijini hapa huku Rais Samia Suluhu Hassan akiwa mgeni rasmi.

Mususa amesema mwaka huu mwelekeo wa maadhimisho ni kuhamasisha ujumuishaji na kuwa huo ndio mwelekeo mwafaka.

"Katika kitabu cha 'Why Nations Fail' cha Daron Acemoglu na James A. Robinson, wamesisitiza ujumishaji kama kiwezeshaji muhimu cha maendeleo ya nchi. Kitabu kinatoa mifano mbalimbali. Katika Afrika kinatoa mfano Botswana (ilivyo fanikiwa) na Zimbabwe (ilivyoshidwa)," amesema Mususa.

Amesema ni vigumu kuzungumzia ujumuishaji kama asilimia kubwa ya wananchi hawashiriki kikamilifu katika shughuli za uchumi.

"Hapa Tanzania tumeona mabadiliko katika miaka ya hivi karibuni, idadi ya kina mama katika uongozi imeongezeka kwa viwango mbalimbali," amesema Mususa.

Amesema nchi kuwa na Rais mwanamke pamoja na mawaziri wanane (wanawake) ni mafanikio ambayo yanahitaji kupongezwa.

Amesema katika hilo kampuni nyingi zimefanya jitihada za kuongeza usawa wa kijinsia katika uongozi huku akiitaka Mwananchi Communications Ltd kujitahidi katika hilo, akitolea mfano wa kampuni mbalimbali ambazo zimefanikiwa katika lengo hili.

"Kwa mfano TBL (Kampuni ya Bia Tanzania)  ina asilimia 58 ya wanaweka katika menejimenti. PwC nimetoka siku nyingi lakini taarifa nilizo nazo ni kwamba akina mama wapo wa kutosha katika uongozi,"  amesema Mususa.