Tyla, Usher wateka BET 2024

Muktasari:

  • Tuzo hizi zinazoandaliwa na Black Entertainment Television (BET), tangu Juni 19, 2001 zinalenga kusheherekea mafanikio ya kazi za Wamarekani Weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji na michezo

Marekani, Usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Peacock huko Los Angeles, Calfornia nchini Marekani kumetolewa tuzo za BET 2024 ambapo Usher Raymond IV na Tyla ndio mastaa waliong'aa zaidi.

Tuzo hizi zinazoandaliwa na Black Entertainment Television (BET), tangu Juni 19, 2001 zinalenga kusheherekea mafanikio ya kazi za Wamarekani Weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji na michezo.

Hata hivyo, mwaka 2010 BET walianza kujumuisha wasanii wa Afrika katika tuzo hizo kupitia kipengele cha 'Best International Act; Africa' ambacho 2018 kilibadilishwa na kuwa 'Best International Act' kikihusisha wasanii wote kutoka nje ya Marekani.

Usher amepokea tuzo ya Heshima ya Mafanikio katika Sanaa, pia ameshinda kama Msanii Bora wa Kiume wa R&B/Pop kwa mara ya tano akiwa ni msanii wa pili aliyeshinda kipengele hicho mara nyingi zaidi nyuma ya Chris Brown aliyeshinda mara saba.

Kwa upande wake Tyla kutoka Afrika Kusini ambaye pia mshindi wa Grammy 2024, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuwania BET ameshinda tuzo mbili sawa na Victoria Monet.

Tyla ameshinda kama Msanii Bora Kimataifa akiwabwaga Asake (Nigeria), Aya Nakamura (Ufaransa), Ayra Starr (Nigeria), Bk’ (Brazil), Cleo Sol (Uingeza), Focalistic (Afrika Kusini) na Karol Conka (Brazil).

Vilevile Tyla aliyetamba na wimbo wake, Water (2023), ameshinda kama Msanii Bora Chipukizi mbele ya 41, 4Batz, Ayra Starr, Bossman Dlow, Fridayy, October London na Sexyy Red.

Kwa matokeo hayo, Tyla anakuwa msanii wa tatu ambaye hakuzaliwa Marekani kushinda kipengele cha Msanii Bora Chipukizi, wengine ni Nicki Minaj aliyezaliwa Trinidad na Sam Smith aliyezaliwa Uingereza.

Msanii mwingine wa Afrika aliyeshinda ni Tems kutoka Nigeria aking'aa kipengele cha Wimbo Bora ya Injili/Uhamasishaji kupitia wimbo wake, Me & U (2023), hii inakuwa ni tuzo yake pili ya BET baada ya kushinda kama Msanii Bora Kimataifa 2022.

Naye Beyonce Knowles ameshinda kipengele cha Chaguo la Watu kupitia wimbo wake, Texas Hold ’Em (2024), hii inakuwa tuzo yake 33 na kuendelea kuwa msanii aliyeshinda tuzo nyingi zaidi za BET kwa muda wote akifuatiwa na Chris Brown aliyeshinda tuzo 19.

Orodha kamili ya washindi wa BET 2024 hii hapa chini.

Album of the year

Killer Mike, Michael — Mshindi

Best female R&B/pop artist

SZA — Mshindi

Best male R&B/pop artist

Usher — Mshindi

Best group

¥$, Ye, Ty Dolla $ign — Mshindi

Best collaboration

Lil Durk feat. J. Cole, “All My Life” — Mshindi

Best female hip-hop artist 

Nicki Minaj — Mshindi

Best male hip-hop artist

Kendrick Lamar — Mshindi

Best new artist

Tyla — Mshindi

Video of the year     

Victoria Monét, “On My Mama” — Mshindi

Video director of the year

Cole Bennett — Mshindi

Dr. Bobby Jones Best Gospel/Inspirational Award

Tems, “Me & U” — Mshindi

Viewer’s choice award

Beyoncé, “Texas Hold ‘Em” — Mshindi                    

Best international act

Tyla (Africa) — Mshindi

Viewer’s choice: Best new international act

Makhadzi (Africa) — Mshindi

BET Her

Victoria Monét, “On My Mama” — Mshindi

Best movie

Bob Marley: One Love — Mshindi

Best actor

Denzel Washington — Mshindi

Best actress

Regina King — Mshindi

YoungStars Award 

Blue Ivy Carter — Mshindi

Sportswoman of the Year Award

Angel Reese — Mshindi

Sportsman of the Year Award

Jalen Brunson — Mshindi.