Saba wafariki dunia ajali ya ambulance na toyo

Mafinga. Watu saba wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali ya gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kugongana na toyo katika eneo la Luganga, lililopo katika Halmashauri ya Mji Mafinga, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.

Akizungumza baada ya kutembelea majeruhi wa ajali hiyo leo Jumamosi, Aprili 19, 2025, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dk Linda Salekwa, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Amesema kuwa taarifa zinaonyesha watu hao walikuwa wanakwenda shambani kufanya kazi, ndipo gari hilo likagongana na toyo hiyo na kusababisha watu hao kufariki dunia na wengine kujeruhiwa.

Endelea kufuatilia Mwananchi.