Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Je, Priscilla ataondoa kivuli cha Vanessa kwa Jux?

JUX Pict

Muktasari:

  • Jux, mwanachama wa kundi la Wakacha lililobamba na wimbo wao, Here We Go (2011), amefunga ndoa na Priscilla ambaye ni binti wa Iyabo Ojo, mmoja wa waigizaji wakongwe huko Nollywood akiwa amecheza filamu zaidi ya 150 tangu mwaka 1998.

Dar es Salaam. Kwa namna harusi ya Jux na Priscilla ilivyoenda huko Nigeria, baadhi ya mashabiki wake wanadai sasa nyoyo zao zimeridhika kwa kile wanachotaja kama kulipwa kisasi kwa aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki huyo kwa takribani miaka sita, Vanessa Mdee.

Jux, mwanachama wa kundi la Wakacha lililobamba na wimbo wao, Here We Go (2011), amefunga ndoa na Priscilla ambaye ni binti wa Iyabo Ojo, mmoja wa waigizaji wakongwe huko Nollywood akiwa amecheza filamu zaidi ya 150 tangu mwaka 1998.

Hata hivyo, swali la wengi ni iwapo Priscilla ataondoa kivuli cha Vanessa katika maisha ya Jux maana kimemsumbua kwa muda mrefu, na kuna hisia kuwa huenda hatua yake ya kwenda kuoa Nigeria ni sehemu ya kupambana na kivuli hicho.

Utakumbuka Jux na Vanessa walikuwa na uhusiano kati ya mwaka 2014 hadi 2019, walifanya mengi pamoja kama kutoa nyimbo mbili zilizofanya vizuri, Juu (2016) na Sumaku (2019), pia kuandaa tamasha lao, Inlove & Money Tour 2018. 

JU 001

Walikutana kwa mara ya kwanza studio ya Bxtra Records, zamani B’Hits ambapo Vanessa ndipo tu alikuwa amesaini lebo, aliyewaweka karibu zaidi ni marehemu Pancho Latino ambaye ndiye mtayarishaji wa wimbo ule wa Wakacha, Here We Go (2011). 

Baada ya kuachana, Jux akawa na Nayika Thongom kutokea Thailand aliyemtumia katika video ya wimbo wake, Unaniweza (2020), huku Vanessa akiwa na Rotimi kutokea Marekani aliyetumia katika video ya wimbo wake, Love Somebody (2020).

Ila uhusiano wa Jux na Nayika haukudumu hata mwaka mmoja kwa kile kinachotajwa kama umbali kati yao, na ndipo ishara za kuteswa na kivuli cha Vanessa zikaanza kuonekana wazi wazi hasa kupitia muziki wake. 

Katika video ya wimbo wake, Sio Mbaya (2020), mwanzo unasikika wimbo, Sumaku (2019) alioshirikiana na Vanessa na ndani yake akionekana mrembo aliyefanana kabisa na Vanessa huku Jux akimwimbia kuwa kwake sio mbaya hata akimpigia simu na kumsalimia.

JU 02

Hilo lilijirudia tena katika wimbo, Lala (2021) alioshirikishwa na Rayvanny, huku Jux alijiachia kabisa akilitaja jina la Vanessa na kudai alishamsahau na hata simu yake alishaizuia (block) kuingia kwake.

Na baada ya Vanessa kuweka wazi ujauzito wake wa kwanza, mara moja Jux akatoa wimbo, Sina Neno (2021) na kumtakia heri katika safari yake ya kuwa mama, pia video yake kamtumia pia mrembo anayefanana na Vanessa.

Utakumbuka Vanessa yupo na Rotimi mwenye asili ya Nigeria tangu 2019, hivyo hatua ya Jux kwenda kuoa nchini humo wengi wanaitafsiri kama amelipa kisasi au bado kivuli cha Vanessa kinamtesa na ndicho kimechochea uamuzi huo.

JU 03

Rotimi ambaye ni muigizaji na mwanamuziki alimvisha pete ya uchumba Vanessa hapo Desemba 2020, wawili hao wanaoishi wote huko Georgia, Marekani, tayari wamejaliwa watoto wawili ambao ni Seven (2021) na Imani (2023).

Katika ndoa yake na Priscilla, chochote atakachofanya Jux watu wataunganisha tu matukio na kuja na picha yao kubwa huku Vanessa akiwa mbele kama mwamuzi wa mchezo husika ambaye anaamua mambo yaende vipi.

Mathalani, Julai 2017 Vanessa akiwa Nigeria alithibitisha kuachana na Jux kwa mara ya kwanza ingawa walikuja kurudiana Desemba katika jukwaa la Fiesta baada ya Q Chief kufanya kazi kubwa katika tamasha hilo.

Miaka nane baadaye, yaani Aprili 2025 Jux anaenda Nigeria kufanya harusi kubwa kifahari na Priscilla tangu waweke wazi uhusiano wao hapo Julai 2024 ikiwa ni miezi michache tangu Jux kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Karen Bujulu.

Kwa upande mwin-gine wapo wanao-amini Jux hajaona Nigeria kwa sababu mume wa Vanessa ana asili ya huko, bali lengo ni kulishika soko lao la muziki kwa kushirikiana na wasanii wa huko, huku ushawishi wa mkewe Priscilla nchini humo ukimsaidia.

JU 04

Tayari Jux ametoa wimbo mpya, God Design (2025) akimshirikisha rapa wa Nigeria, Phyno, lakini hatua hii kubwa bado inaonekana inapita mule mule kwa Vanessa ambaye awali alishafanya kazi na baadhi ya wasanii wa nchi hiyo.

Mwaka 2013 Vanessa alishirikiana na Burna Boy katika jukwaa la Coke Studio Africa, kisha akatoa wimbo, Kisela (2017) akiwa na Mr. P kutoka kundi la P-Square, pia alishirikiana na Reekado Banks katika wimbo, Bambino (2018).

Hivyo, kutokana kila analofanya Jux linaonekana kuwa chini ya kivuli cha Vanessa, basi Priscilla ana jukumu la kujenga historia mpya kwa msanii huyo kama alivyosema katika wimbo ‘Here We Go’ kuwa... Lucky never before. This is how we do, ni time ya ku-make dow.