Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diddy ang'atuka katika kampuni yake kisa tuhuma za ubakaji

Muktasari:

Habari hizi zinakuja takribani wiki mbili baada ya aliyekuwa mpenzi wa Diddy, Cassie kuwasilisha kesi akimtuhumu msanii huyo wa Hiphop kwa ubakaji, unyanyasaji na biashara ya ngono wakati wa uhusiano wao wa muongo mmoja.

Rapa wa Marekani, Sean Combs 'Diddy' amejiuzulu kama Mwenyekiti wa Revolt Media, kampuni ya habari aliyoianzisha mwaka 2013, uamuzi huo unakuja baada ya kukabiliwa na tuhuma kadhaa za ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia.

Revolt ndio wametoa taarifa hiyo na kueleza kuwa ingawa Diddy hakuwa na jukumu la kazi la kila siku katika biashara, uamuzi huu unasaidia kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inabaki na dhamira yake ya kutengeneza maudhui ya maana.

"Lengo letu siku zote limekuwa kuonyesha kujitolea kwetu kwa safari ya pamoja ya Revolt ambayo haichochewi na mtu yeyote bali kwa juhudi za pamoja na maadili ya timu yetu nzima, kwa niaba ya kuendeleza, kuinua na kupigania utamaduni wetu," imeeleza taarifa yao.

Habari hizi zinakuja takribani wiki mbili baada ya aliyekuwa mpenzi wa Diddy, Cassie kuwasilisha kesi akimtuhumu msanii huyo wa Hiphop kwa ubakaji, unyanyasaji na biashara ya ngono wakati wa uhusiano wao wa muongo mmoja.

Ingawa Diddy amekanusha madai hayo, walisuluhisha suala hilo nje ya mahakama, Diddy amesema wameamua kutatua suala hilo kwa amani na kumtakia kila la heri Cassie na familia yake.

"Nimeamua kutatua suala hili kwa amani, nataka kuwashukuru familia yangu, mashabiki na wanasheria wangu kwa msaada wao madhubuti," amesema Cassie ambaye ni mwimbaji pia.

Ila tayari wanawake wengine wawili wamejitokeza wakimtuhumu kwa madai sawa na hayo, mmoja ambaye jina lake halikujulikana amedai kuwa Diddy na mwenzake Aaron Hall walimbaka yeye na rafiki yake ambaye hajatambuliwa mnamo mwaka 1990/91.

Hata hivyo, msemaji wa Diddy aliyaita madai hayo ya kutunga katika taarifa yake aliyotuma katika mtandao wa Pagesix, amesema wanatunga uongo ili kuvuna fedha kwa Diddy na kuwataka watu kuwa makini.

"Kwa sababu ya umaarufu na mafanikio ya  Combs, analengwa kwa urahisi na washtaki wasiojulikana wanaosema uwongo kwa dhamiri ya kupata manufaa ya kifedha, umma unapaswa kuwa na shaka na usikimbilie kukubali madai haya ya uwongo," amesema.

Kuna madai kuwa Revolt Media iliwapiga marufuku wafanyakazi wake kuandika chochote kibaya kuhusu Diddy na marafiki zake maarufu. Hata hivyo, Revolt iliripoti kuhusu wakili wa Rapa huyo ambaye amesema kwamba kitendo cha mteja wake kusuluhisha mara moja suala lake na Cassie haikuwa kwa njia yoyote ya kukiri kosa.