Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waokota taka hatarini kupata magonjwa haya

Muktasari:

  • Ingawa kazi yao ina manufaa kwa jamii kwa kupunguza uchafu na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa mazingira, waokota taka mijini wanakutana na hatari nyingi ambazo ni muhimu kushughulikiwa ili kuhakikisha usalama wao.

Dar es Salaam. Kukaa sehemu isiyo na hewa, kutumia dawa za kulevya ni miongoni mwa sababu zilizotajwa kuwa chanzo cha maambukizo ya ugonjwa wa kifua kikuu, kwa watu wanaojihusisha na shughuli za kuokota taka mijini.

Hayo yamebainishwa kwenye semina ya mafunzo ya usalama na afya kwa waokota taka, iliyoandaliwa na Taasisi ya Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira ya Juza, iliyowakutanisha waokota taka mwishoni mwa hivi karibuni jijini Dar es Saalam.

Peter Renatus kutoka Ofisi ya Tokomeza Kifua Kikuu na Ukimwi Tanzania (Tokikuta), anasema waokota taka wako hatarini zaidi kupata kifua kikuu kutokana na mazingira wanayoishi.

"Waokota taka walio wengi wanatumia dawa za kulevya na watu wenye hatari ya kupata kifua kikuu, ni watu wanaotumia dawa za kulevya, kwasababu wanajificha halafu wanakuwa wengi na hakuna hewa ya kutosha.

"Kifua Kikuu kinaambukizwa kwa njia ya hewa kwahiyo mmoja wao akikohoa, ina maana na wengine wote wanavuta vimelea na kutokana na afya zao, ni rahisi kuugua," anasema Renatus.

Anasema mkakati uliopo kuwaokoa kundi hilo kwa kushirikiana na taasisi ya Juza, ni kuwasimamia kumaliza dozi ya miezi sita pale wanapogundulika na maambukizi.

"Wakija asubuhi kabla ya kuanza kuokota taka wanakunywa dawa hadi pale watakapomaliza miezi sita," anasema.

Anawashauri waokota taka kutokaa sehemu yenye msongamano wa watu wengi, akionekana mmoja wao ana maambulizi basi awahi matibabu.

Akizungumza na Mwananchi, muokota taka eneo la Kariakoo, Joseph Mayowela anasema suala la afya linapaswa kuwa la kwanza katika shughuli zao za kila siku ingawa kuna hatari ya kupata maradhi ikiwemo ya milipuko.

"Nikiwa kazini huwa navaa glovu na buti ngumu pamoja na barakoa kuepuka hatari ya kupata maradhi. Nawashauri na wenzangu wazingatie afya," anasema Mayowela.

Naye Sakina Mfaume anasema changamoto iliyopo kwake ni uchafu ambao unambabua mikono yake kwakuwa havai vizuia mikono mara zote.

"Niliwahi kubabuka mikono na vidole kutokana na kuokota taka jalalani, lakini pia huwa navuta hewa chafu kiasi cha kushindwa kuhema vizuri,"anasema Meshack Dugange , muokota taka Kariakoo.

"Sasa hivi naumwa kifua kikuu, kuna wakati unaweza ukavuta hewa mbaya ukifungua machupa yenye kemikali," anasema Dugange.


Hatari zaidi zinazowakabili

Ingawa kazi yao ina manufaa kwa jamii kwa kupunguza uchafu na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa mazingira, waokota taka mijini wanakutana na hatari nyingi ambazo ni muhimu kushughulikiwa ili kuhakikisha usalama wao.

Hatari hizi zipo katika nyanja za kiafya, kimazingira, na kijamii, na pia kuna changamoto za kisheria na kijamii zinazohusiana na kazi hii.

Hatari ya kwanza inayowakabili waokota taka ni ile ya afya. Waokota taka wanakutana na mazingira yenye vichafuzi vingi, ikiwa ni pamoja na mabaki ya kemikali, sumu, taka za viwandani na taka nyingine hatari, ambazo zinaweza kusababisha magonjwa mbalimbali. Kwa mfano, waokota taka wanaweza kuathirika na magonjwa ya ngozi kutokana na kugusa taka zinazoharibika au zilizochafuka, kama vile vidonda vya ngozi au maambukizi.

Aidha, takataka nyingi zinajumuisha mabaki ya vyakula au vitu vingine vinavyoweza kuzalisha bakteria na virusi ambavyo vinaweza kusababisha magonjwa kama vile kipindupindu, homa ya matumbo, na kuharisha.

Taka za kemikali, kama vile mafuta ya magari, rangi, au viambata vya sumu, zinaweza kuwa na madhara makubwa kwa afya ya waokota taka, ikiwa ni pamoja na kuathiri mapafu, mfumo wa fahamu, na hata kusababisha saratani.

Hatari nyingine inayowakabili waokota taka ni ile ya ajali. Katika miji mingi, waokota taka wanaweza kukutana na maeneo hatari ambayo hayajasimamiwa vizuri. Kwa mfano, waokota taka mara nyingi hutembea barabarani au katika maeneo yasiyo salama ambapo wanakutana na magari, pikipiki, na mifumo ya usafiri wa umma.

Ajali za barabarani, kama vile kugongwa na magari, ni hatari kubwa kwa waokota taka mijini. Aidha, waokota taka wanaweza kupata ajali kutokana na kushika au kubeba vitu vizito, vyenye ncha kali au vyenye maudhui ya hatari, kama vile shaba, kigae, au vipande vya chuma, ambavyo vinaweza kusababisha majeraha makubwa.

Waokota taka pia wanakutana na hatari ya kiakili na kijamii. Kazi ya kukusanya taka mara nyingi hufanywa katika mazingira magumu na ya kujitolea, na waokota taka mara nyingi hawana ulinzi wa kisheria au haki za kimsingi.

Wengi wao wanakutana na unyanyapaa na ubaguzi kutoka kwa jamii, kwani kazi wanayofanya inachukuliwa kama ya chini na isiyo ya heshima. Unyanyapaa huu unaweza kusababisha waokota taka kujihisi kutengwa na jamii na kupunguza heshima yao binafsi.

Aidha, waokota taka mara nyingi hawawezi kupata huduma bora za afya, elimu, au haki za kisheria, kwani wengi wao wanaishi katika hali ya umasikini na hawana uwezo wa kumudu gharama za huduma muhimu.

Kwa upande mwingine, waokota taka wanakutana na hatari ya mazingira, hasa wakati wanapokuwa wakikusanya taka kutoka maeneo yasiyosafi au hatari. Taka zinazozunguka katika mazingira ya mijini mara nyingi ni za aina nyingi, na baadhi ya takataka hizi zinaweza kuwa na kemikali hatari au kuwa na uchafuzi wa mazingira.

Waokota taka wanaweza kukutana na maeneo ya taka yaliyosambaa, kama vile mifuko ya plastiki, vyuma vilivyoharibika, na taka za sumu, ambazo zinaweza kuchafua maeneo ya kijiji au jiji.

Pia, taka zinazochafua mazingira zinaweza kuathiri vyanzo vya maji na udongo, jambo ambalo linawaweka waokota taka katika hatari ya kupata magonjwa ya kuambukiza kutoka kwa vyanzo vya maji visivyo salama.


Tahadhari gani wachukue?

Ili kujipepusha na hatari hizi, waokota taka wanapaswa kuchukua tahadhari kadhaa. Kwanza, wanahitaji kuvaa vifaa vya kinga vinavyofaa, kama vile mavazi ya kinga, miwani ya macho, glovu, na viatu vya kinga.

Hii itawasaidia kuepuka majeraha na maambukizi kutoka kwa takataka hatari. Vilevile, matumizi ya vifaa vya kinga kama vile barakoa ya kupumua vitasaidia kuwalinda waokota taka dhidi ya vumbi na vichafuzi vya hewa ambavyo vinaweza kusababisha matatizo ya mapafu.

Waokota taka pia wanapaswa kuhakikisha kuwa wanachukua tahadhari za kiafya, kama vile kunawa mikono mara kwa mara, kutumia dawa za kuua vijidudu na kuepuka kugusa moja kwa moja taka zinazoweza kuwa na maambukizi.

Hatari ya ajali inaweza kupunguzwa kwa waokota taka kuzingatia usalama wa barabarani. Wanaweza kuvaa mavazi ya kung'aa au kutumika kwa miwani ya kuonekana mbali ili kuongeza ufanisi wa ulinzi wao dhidi ya magari na vifaa vya usafiri vingine.

Pia, waokota taka wanapaswa kuepuka maeneo hatari kama vile mitaa yenye usafiri mwingi na badala yake kutumia njia salama na zile zenye mwanga wa kutosha. Kwa wale wanaoshughulika na vitu vizito, wanahitaji kujua mbinu sahihi za kubeba vitu ili kuepuka majeraha ya mgongo au mikono.

Kwa upande wa kijamii, ni muhimu kwa waokota taka kutafuta msaada kutoka kwa jamii na Serikali ili kuhakikisha kuwa wanapata haki zao na ulinzi wa kisheria.

Serikali na mashirika ya kiraia yanaweza kusaidia kwa kutoa elimu kuhusu usafi wa mazingira, kutoa vifaa vya kinga, na kusaidia kuanzisha mifumo ya kuzingatia haki za waokota taka.

Zaidi ya hayo, Serikali inaweza kuweka sera zinazolinda haki za waokota taka na kuhakikisha kuwa wanapata matibabu ya afya, elimu, na huduma za kijamii.


Harakati za Juza

Mkurugenzi Mtendaji wa  Juza, Nassib  Kitabu anasema waokota taka ni watu muhimu katika kutunza  mazingira,  kutokana na shughuli wanayofanya.

Anasema kutokana na umuhimu wao, wamewakutanisha kwa ajili ya kuwapatia vifaa kinga, elimu ya kujikinga na maradhi huku lengo likiwa kuwafikia waokota taka takribani 600 jijini Dar es Salaam.

"Naiomba Seirkali na wadau mbalimbali waunge mkono juhudi hizi za kuwasaidia hawa vijana kuepuka changamoto za kiafya ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya na usalama wao wa kiafya,"anabainisha.

Anasema mkakati uliopo wanawapa dawa za kifua kikuu kwenye kituo cha Juza kila siku pamoja na lishe. Kuwatengenezea mipango ya kiuchumi itakayowaweka mbali na matumizi ya dawa za kulevya.