Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Leo wa XIV ndiye Papa mpya wa Kanisa Katoliki

Vatican. Kardinali Robert Prevost (69) kutoka Marekani amechaguliwa kuwa Papa mpya wa 267 akichagua jina la Leo wa XIV ikiwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kupatikana kutoka Taifa hilo.

  

Zaidi ya saa moja baada ya moshi mweupe kufuka ikiwa ni kupatikana kwa Papa mpya alijitokeza kwenye dirisha la baraka la Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Kardinali Shemasi Dominique Mam-berti na kutangaza, ‘Tunaye Papa.’

Hatua hiyo imefikiwa baada ya siku mbili za kupiga kura na akidi ya theluthi mbili muhimu kwa uchaguzi huo kufikiwa.

Katika siku ya pili ya mkutano mkuu wa uchaguzi wa Papa mpya leo Mei 8, 2025 saa 12:07 jioni (saa 1:07 usiku saa za Afrika Mashariki na Kati) imeshuhudiwa moshi mweupe kupitia dohani katika kanisa dogo la Sistine kuashiria kuwa Papa amepatikana.

Kengele zilisikika zikigongwa wakati wa tukio hilo ikiwa ni sehemu ya shangwe za kupatikana Papa mpya,  makardinali 133 wamemchagua mrithi wa Papa Francis aliyefariki dunia Aprili 21, 2025.

Umati wa watu, wapatao 20,000 waliofika kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro kumkaribisha Papa mpya, walilipuka kwa shangwe na nderemo wakipeperusha bendera za nchi kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Baadhi ya watu walioshuhudia kufuka kwa moshi huo walitumia simu zao za mkononi kuchukua kumbukumbu ya tukio hilo.

Moshi mweupe ulitanguliwa na mweusi uliofuka kwa nyakati tofauti mara mbili leo asubuhi na jana Mei 7, 2025 usiku.

Katika historia ya kanisa, mkutano uliofanyika kwa muda mfupi unakadiriwa kuwa saa 10 uliofanyika mwaka 1503 baada ya kifo cha Papa Pius III. Makardinali walikutana na kumchagua Papa Julius II.

Mkutano mrefu zaidi katika historia ulichukua takribani miaka mitatu (siku 1,006) alipochaguliwa Papa Gregory X mwaka 1271.

Papa Leo XIV, mpenda mchezo wa tenisi aliyejulikana pia kwa jina la ‘Bob’ anatajwa kuwa mtu ataka-yeendeleza maono ya Papa Francis.

Amefanya kazi kwa miaka mingi nchini Peru na alikuwa chaguo maarufu miongoni mwa makardinali wa Amerika ya Kusini na Amerika Kaskazini, ingawa amekuwa kimya kuhusu maoni yake juu ya masuala kama vile makasisi wanawake na ndoa za jinsia moja.

Baada ya kutangazwa akiwa kwenye dirisha la Baraka, Papa Leo XIV aliwashukuru makardinali waliomchagua wakati wa mkutano uliodumu kwa siku mbili.

"Tunaweza kutembea pamoja kuelekea kwenye makao yale ambayo Mungu ametutayarishia," amesema.

Ametoa baraka kwa umati uliofurika kwenye Uwanja wa Mrakatifu Petro ambao wakati wote ulikuwa ukishangilia.

Papa Leo XIV ametoa ujumbe wa amani akisema, "Mungu anatupenda sote, bila masharti.

"Ubinadamu unamuhitaji Kristo kama daraja la kufikiwa na Mungu na upendo wake. Tusaidie, na tusaidiane, kujenga madaraja," amesema.