Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Papa mpya bado hajapatikana, Moshi mweusi wafuka tena

Muktasari:

  • Makardinali saa 11:30 jioni wataendelea na upigaji wa kura.

Vatican. Katika siku ya pili ya mkutano mkuu wa uchaguzi wa Papa mpya leo Mei 8, 2025 umeshuhudiwa moshi mweusi kupitia dohani katika kanisa dogo la Sistine kuashiria bado hajapatikana.

Makardinali 133 bado hawajamchagua mrithi wa Papa Francis aliyefariki dunia Aprili 21,2025.

Ikiwa ni mwishoni mwa upigaji kura mara ya pili, moshi mweusi ulitoka kwenye dohani ya kanisa hilo saa 5:51 asubuhi (saa 6:51 saa za Afrika Mashariki na Kati).

Watu wapatao 15,000 waliokusanyika katika Uwanja wa Kanisa la Mtakatifu Petro walishuhudia moshi huo ukifuka, wengi wakiwa wameshikilia simu mikononi.

Tukio hilo lilirekodiwa na kurushwa na vituo mbalimbali ya luninga duniani.

Mchakato wa uchaguzi ulianza jana Mei 7, 2025. Kwa mara ya kwanza moshi mweusi ulifuka kutoka kwenye dohani la kanisa hilo saa 3:00 usiku (saa 4:00 saa za Afrika Mashariki na Kati) wa Mei 7, kuashiria Papa wa 267 bado hajapatikana.

Umati katika Uwanja wa Mtakatifu Petro umeendelea kuwa na matumaini, ukitazama kwa macho yaliyojaa imani na matarajio kusubiri ishara itakayotangaza mwanzo wa enzi mpya kwa kanisa.

Kwa mujibu wa Vatican News, takriban watu 45,000 walikuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kusubiri tangazo hilo jana Mei 7.

Miongoni mwao alikuwa Shemasi Nicholas Nkoronko kutoka Tanzania aliyeliambia Vatican News kuwa: "Jukumu letu hapa ni kusali na kuungana na Wakristo wengine, Wakatoliki wengine, kumwomba Roho Mtakatifu aongoze mchakato mzima. Popote anapotoka Papa mpya."

Shemasi Nkoronko amesema: "Iwe ni Afrika, Asia, Amerika, tunachohitaji ni Papa. Tunahitaji Papa ambaye ataliongoza kanisa na atakuwa mchungaji wa kanisa."


Ratiba ya Alhamisi

Leo Alhamisi Mei 8, 2025, makardinali wapigakura walikusanyika katika Jumba la Kitume kuadhimisha misa na masifu ya asubuhi katika kanisa dogo la Pauline.

Baadaye saa 3:15 (saa 4:15) waliingia katika kanisa dogo la Sistine kusali masifu ya tatu na kisha kuendelea kupiga kura.

Kwa mujibu wa ratiba, chakula cha mchana kilitarajiwa kuliwa saa 6:30 (saa 7:30) mchana katika Nyumba ya Mtakatifu Marta ambako saa 9:45 alasiri (saa 10:45) walitakiwa kuondoka hadi Jumba la Kitume.

Saa 10:30 jioni (saa 11:30) wataingia tena katika kanisa dogo la Sistine ikielezwa kura mbili zaidi za mwisho zinatarajiwa kupigwa.

Inatarajiwa saa 1:30 usiku (saa 2:30) maadhimisho ya masifu ya jioni yatafanyika.

Uchaguzi unaendelea kukiwa hakuna muda maalumu uliowekwa hadi pale Papa mpya atakapopatikana kutegemea idadi ya kura zinazohitajika kufikia theluthi mbili.

Mkutano uliofanyika kwa muda mfupi unakadiriwa kuwa saa 10 ulifanyika mwaka 1503 baada ya kifo cha Papa Pius III. Makardinali walikutana na kumchagua Papa Julius II.
Mkutano mrefu zaidi katika historia ulichukua takribani miaka mitatu (siku 1,006) alipochaguliwa Papa Gregory X mwaka 1271.