Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SMZ kukabiliana upandaji bei za vyakula

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi akizungumza na wafanyabiashara na watendaji wa Serikali Ikulu Zanzibar leo Septemba 25, 2023.

Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema Serikali amesema Serikali inafanya jitihada kubwa kudhibiti mfumko wa bei za bidhaa hususani vyakula huku aliwataka wafanyabiashara kutopandisha bei hizo.

Dk Mwinyi ametoa kauli hiyo leo jioni Septemba 25, 2023 Ikulu, Zanzibar alipokutana na wafanyabiashara, wazalishaji wanaoingiza bidhaa na mizigo na wadau wote wa biashara zikiwemo taasisi za Serikali na binafsi kujadili mustakabali wa bei za bidhaa kisiwani humo.

Amewataka wafanyabiashara hao kutopandisha bei za vyakula hususani sukari ambao ushuru wake upo chini ikilinganishwa na sehemu nyingine yoyote. Kwasasa kilo moja ya sukari ni Sh3,000.

Dk Mwinyi aliwaeleza wafanyabiashara hao kuwa karibu na kuzungumza na Serikali wakati wote kunapotokea matatizo badala ya kuwapandishia bei wananchi maana wao ndio waathirika wakubwa.

"Kila inapotokea changamoto tukae mezani tuangalie namna bora ya kushughulika nayo," amesema.

Akizungumzia sarafu ya Dola, Rais Mwinyi amezitaka mamlaka husika kutoa kipaumbele kwa wafanyabiashara wa chakula ili kuwaondoshea wananchi usumbufu wa uhaba wa chakula nchini.

Katika hatua nyengine, Mkuu wa huo wa nchi, amewataka wafanyabiashara hao kuangalia uwezekano wa kuagiza bidhaa kwa pamoja na kuingiza nchini kwa wakati ili kuepuka gharama za usafirishaji na kuchelewa kuingiza.

“Lazima kutafutwe njia ya kushushia vyakula moja kwa moja Pemba, mshirikiane kuchukua meli kutoka Bandari ya Malindi hadi Pemba, kutafutwe ufumbuzi kwa njia yoyote ili kupunguza gharama za bidhaa madukani,” amesema Dk Mwinyi.

Akizungumzia mabadiliko kwa Shirika la Bandari la Zanzibar, Dk Mwinyi amesema mabadiliko yoyote yanachangamoto zake, hivyo amewataka wafanyabiashara hao kutoa ushirikiano kwa uwekezaji mpya wa bandari hiyo na kuuagiza uongozi wa shirika hilo kusimamia changamoto zinazojitokeza kwa kipindi hiki cha awali cha mkataba na wawekezaji.

Bandari ya Malindi upande wa mizigo amekabidhiwa mwekezaji Kampuni ya AGL kutoka Ufaransa. Hata hivyo tangu akabidhiwe rasmi kuendesha bandari hiyo Septemba 18, 2023 zimeibuka changamoto kadhaa ikiwemo wafanyabiashara kulalamikia ongezeko la ushuru na utaratibu wa kuegesha meli.