Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Mwinyi alitaka kundi la G77 kutosubiri misaada

Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi kakihutubia mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa kundi la G77 pamoja na China, unaofanyika Havana, Cuba

Muktasari:

  • Rais Mwinyi amekumbusha namna nchi zinazoendelea zilivyoathirika vibaya na janga la maradhi ya Uviko-19, kwa kupanda kwa   bidhaa, mizozo ya kisiasa na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

Unguja. Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi amesema Sayansi, teknolojia na ubunifu ni mambo muhimu kwa nchi zinazoendelea hasa katika masuala ya uchumi wa kijamii hivyo kuzitaka zisibweteke kusubiri misaada kutoka mataifa tajiri.

Amesema nchi hizo zinaweza kubadili maisha ya watu wake kupitia sekta muhimu kama ya kilimo, nishati na elimu.

Dk Mwinyi ameyasema hayo jana Septemba 15 alipohutubia katika mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa kundi la G77 pamoja na China akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan unaofanyika Havana, Cuba.

Dk Mwinyi amekumbusha namna nchi zinazoendelea zilivyoathirika vibaya na janga la maradhi ya Uviko-19, kwa kupanda kwa   bidhaa, mizozo ya kisiasa na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

Katika hotuba yake amekumbushia namna nchi zilizoendelea zilivyobaniwa teknolojia ya kutengeneza chanjo nchi za mataifa ya kusini na kuzinyima msaada wa kiteknolojia ili ziweze kutengeneza chanjo.

 “Hali hiyo iliyosababisha kampuni za utengenezaji dawa ya mataifa tajiri kujipatia faida kubwa kwa kuziuzia nchi masikini chanjo ya Uviko-19,” amesema.

Amesema hizo ni baadhi ya changamoto zilizosababisha kupanda kwa gharama za maisha na kudhoofisha jitahada za kujikwamua kiuchumi kwa nchi zinazoendelea.

Amesema nchi za kundi la G77 na China wachukulie hayo yote kama somo na zisibweteke kusubiri msaada kutoka mataifa tajiri, na huo ndio wakati wa kusema imetosha.