Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mwinyi: Tutayafanyia kazi mapendekezo ya haki jinai

Mwenyekiti wa Tume ya maboresho ya mifumo ya Taasisi za haki jinai, Jaji Mstaafu Othman Chande akimkabidhi Rais Hussein Mwinyi ripoti ya tume hiyo Ikulu Zanzibar.

Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ameahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya maboresho ya mifumo ya taasisi za haki jinai ambayo itatoa mwelekeo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Tanzania Bara.

 Dk Mwinyi ameyasema hayo leo Septemba 9, 2023 Ikulu, Zanzibar alipokutana na tume hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Mstaafu Mohamed Othman Chande na Makamu Mwenyekiti Balozi Ombeni Sefue walipomkabidhi ripoti ya tume hiyo.

Amesema Serikali zote mbili, SMZ na SMT, zimeyapokea mapendekezo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi kwa kina ili kuleta mabadiliko na mageuzi makubwa kwa nia ya kupatikana kwa haki nchini.

Alisema utekelezaji wa mapendekezo hayo kwa kiasi kikubwa unaendana na kutegemeana na taasisi zote za haki jinai za Bara na Zanzibar.

“Bila shaka ni sahihi kabisa lazima kuwe na kubadilishana ujuzi na uzoefu, ushirikiano wa karibu. Tutayafanyia kazi mapendekezo yote,” amesema Dk Mwinyi.

Dk Mwinyi alizungumzia ushirikiano mzuri uliopo baina ya taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa ya Zanzibar (Zaeca) na ya kupambana na dawa za kulevya, zimepata msaada wa kujengewa uwezo na wenzao kutoka Tanzania Bara kwa kupewa mafunzo.

“Bila shaka ni sahihi kabisa lazima kuwe na kubadilishana ujuzi na uzoefu, ushirikiano wa karibu” alisifu Dk Mwinyi.

Kuhusu mahakama ya rufani kufanya kazi zake Zanzibar, amesema tayari suala hilo linashughulikiwa pamoja na kuisifu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuongeza nguvu kwenye ujenzi wa miundombinu ya Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Naye, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Chande, alimueleza Dk Mwinyi kwamba tume imefanikiwa kuzifanyia kazi changamoto za taasisi 15 zilizopendekezwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikiwemo Jeshi la Polisi, Ofisi ya taifa ya Mashitaka, Jeshi la Magereza.

Taasisi nyengine ni mamlaka ya kuzuia na kupambana na Rushwa, Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya, Mahakama ya Tanzania, kitengo cha kudhibirti fedha haramu Uhamiaji, Mkemia Mkuu wa Serikali na taasisi nyengine zinazohusu masuala ya jinai.

Kazi kubwa iliyofanywa kwa kutathmni ushirikiano wa taasisi hizo na kuangalia nidhamu, mifumo ya ajira, viwango vya weledi, tume ya upandishaji vyeo, ufanisi uhusiano, nidhamu, ufanisi matumizi ya teknolojia na motisha.

Tume ya maboresho ya mifumo ya taasisi za haki jinai imeundwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Januari 31 mwaka huu na ilianza kazi zake Februari kwa lengo la kutathmni mifumo ya haki jinai na kutathmini taasisi za haki jinai.