Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabadiliko mfumo haki jinai yaja, Tume haina shaka na Rais Samia

Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya Habari nchini wakizungumza kwenye Mkutano kati yao na Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo 20 Julai, 2023.

Dar es Salaam. Siku tano tangu Tume ya Haki Jinai kuwasilisha ripoti yenye mapendekezo kadhaa yanayolenga kuhuisha mfumo wa haki jinai nchini, imesema haina mashaka na utekelezwaji wa mapendekezo hayo kutokana na dhamira na utashi alionao mkuu wa nchi.

Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam leo Julai 20, 2023; Katibu wa tume hiyo Balozi Ombeni Sefue amesema sambamba na hilo, ukuaji wa teknolojia na uchumi pia ni sababu tosha ya utekelezwaji wa mapendekezo hayo.

Balozi Sefue ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi wakati wa utawala wa Serikali ya awamu ya nne na baadaye awamu ya tano, amesema Rais Samia Suluhu Hassan anataka kuona haki za wananchi zinalindwa.

“Utashi mkubwa wa kisiasa alionao Rais Samia, ukuachi wa teknolojia na uchumi, ni miongoni mwa sababu zinazotupa imani kwamba mapendekezo ya tume hii yatakatekelezwa,” alisema.

Baadhi ya mapendekezo ya tume hiyo, ni yale yanayohusiana na matumizi ya amri ya kukamata, hasa zitolewazo na wakuu wa mikoa na wilaya bila kuzingatia matakwa ya sheria, ambapo tume inata mamlaka hiyo itumike kwa kufuata zile sheria.

Jambo jingine ni uwepo wa taasisi nyingi zenye sura ya kijeshi, kama ambavy imefafanuliwa na mmoja wa wajumbe wa tume hiyo, ambaye pia aliwahi kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Balozi Ernest Mangu.

“Na usimamizi wa sheria siku zote haufanywi kwa mtutu wa bunduki, kwa hiyo zile taasisi nyingine zinazotekeleza jukumu la kipolisi zinapaswa kuzingatia misingi ya kazi ya Polisi,” amesema Balozi Mangu na kuongeza;

“Sasa wewe upo tu unapokea wageni umevaa magwanda sasa si unatisha watu? Maana yake tulichokuwa tunaeleza ni wananchi wanasema mbona hawa wanatutisha, maana ukienda kwenye misingi ya kazi ya polisi ni kutengeneza mazingira mazuri na jamii.”

Msingi wa kuepuka matumizi ya silaha na kutisha wananchi alisema ni kuifanya jamii iwe na mahusiano yatakayowezesha kujitolea katika kutoa taarifa za uhalifu na mambo mengine.

“Ili kupunguza matumizi ya nguvu tukasema tuanze kuondoa ile sura ya jeshi katika kazi yote ya usimamizi wa sheria na tulipokuwa tunazungumza na wadau hata wanajeshi walitwambia wenyewe, ndiyo wanaotoa mafunzo kwa hawa wa Jeshi Ussu.

“Na wanajeshi wenyewe walituambia wao hawajafundishwa kusimamia sheria, wamefundishwa kuuwa adui kwa hiyo hawa wanapokwenda kupata hayo mafunzo maana yake muhalifu wanamuona kama adui yao,” ameeza mjumbe huyo na kuongeza;

“Kwa hiyo hata namna ya ukamataji, wao wanamkamata mtu kama adui wakati mwingine pengine huyo ‘mhalifu’ hajatenda hilo kosa, kuendelea kuwa na taswira za kijeshi inaleta mahusiano yasiyo mazuri kati ya vyombo vyetu na wananchi.”

Akizungumzia hilo, Balozi Sefue amesema kuwa mapendekezo hayo, hayana dhamira ya kupunguza nguvu ya jeshi lolote, lakini kinachopendekezwa ni kuwafanya wale wasio kwenye majukumu ya kijeshi, kutokuwa na ulazima wa kuvaa magwanda.