Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huyu ndiye amechukua nafasi ya Arafat Haji PBZ

Muktasari:

  • Arafat Haji amedumu kwenye nafasi hiyo kwa mwaka mmoja, kwa sasa amechukua fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Shaurimoyo.

Unguja. Rais wa Zanzibar amemteua Fahad Soud Hamid kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said na kutumwa kwa vyombo vya habari leo Juni 30, 2025, uteuzi huo unaanza kesho Julai mosi, 2025.

"Kabla ya uteuzi huo, Fahad alikuwa Mkurugenzi msaidizi, Idara ya Fedha katika shirika la Marekani la msaada wa Maendeleo ya Kimataifa (Usaid), Tanzania," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Mkurugenzi huyo mpya anachukua nafasi ya Arafat Haji aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo kwa takriban mwaka mmoja tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo Mei 10, 2024.

Arafat ambaye pia ni Makamu wa Rais wa timu ya mpira ya Yanga, ameshachukua fomu kuomba ridhaa ya kugombea ubunge Jimbo la Shaurimoyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM ).