Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia ateua wapya yumo Dk Maghembe

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan, amewateuwa viongozi mbalimbali na kuwahamisha baadhi yao.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Dk Grace Maghembe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya.

Kabla ya uteuzi Dk Maghembe alikuwa Mganga Mkuu wa Serikali tangu alipoteuliwa na Rais Samia kushika nafasi hiyo, Januari 17, 2025.

Na sasa, anamrithi Dk Seif Shekalaghe ambaye anakuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria.

Uteuzi huo ni mwendelezo wa kupanda nafasi mbalimbali kwa Dk Maghembe. Mwanataaluma huyo wa Afya, aliwahi kuwa ofisa katika Shirika la Afya Duniani, Geneva nchini Uswisi.

Aliingia serikalini akiwa daktari katika Hospitali ya Amana, baadaye akateuliwa kuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Alipandishwa tena kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais (sasa Waziri Mkuu), Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia afya.

Taarifa ya uteuzi wa Dk Maghembe na wenzake, imetolewa leo, Ijumaa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka na kutiwa saini na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bakari Machumu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Dk Shekalaghe amehamishwa kutoka Wizara ya Afya na kwenda Wizara ya Katiba na Sheria.

Dk Shekalaghe anachukua nafasi ya Dk John Jingu, aliyeteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama.

Pia, Charles Kadonya, ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki.

Kadonya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Stephen Mbundi aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Machi 2026.

Mwingine aliyeteuliwa ni Profesa Verdiana Masanja, anayekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (Tafori).

Taarifa hiyo inasema tarehe ya uapisho wa wateule wote hao itatangazwa baadaye.