Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zitto ambwaga Nondo kura za maoni ubunge Kigoma Mjini

Dar es Salaam. Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameibuka kidedea katika mchakato wa kura za maoni za kuwania Jimbo la Kigoma Mjini uliofanyika jana Jumanne Agosti 12, 2025.

Katika mchakato huo uliofanyika mkoani Kigoma, Zitto ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya ACT Wazalendo, alipata kura 228 dhidi ya 37 alizozipata Nondo ambaye ni mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya chama hicho. Jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 269 kati ya hizo, nne ziliharibika.

Kwa matokeo hayo, Zitto ambaye ni mbunge wa zamani wa jimbo hilo, anasubiri kupendekezwa kamati kuu ya chama hicho, ili kuchukua fomu za uteuzi zitakazoanza kutolewa kesho Alhamisi Agosti 14,2025  na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Leo Jumatano Agosti 13, 2025 Mwananchi Digital lilimtafuta Katibu wa Idara ya Oganaizesheni wa ACT Wazalendo, Shaweji Mketo aliyesema kwa sasa yupo ‘busy’ kusimamia chaguzi zingine zinazoendelea katika majimbo mbalimbali.

“Naomba nikupigie baadaye nitakupa matokeo yote, bado tunaendelea kuyachakata hapa,” amesema Mketo ambaye pia ni mtiania wa ubunge wa Kilwa Kaskazini mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa Ado, majimbo ya Kivule, Chamazi, Kinondoni jana yalitarajiwa mchakato wa kura za maoni ili kuwapata watiania watakaopitishwa katika kikao cha kamati kuu ya chama hicho kitakachoketi siku chache zijazo.