Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sina kinyongo na Lissu, nikiwa Rais tutashirikiana: Mwalimu

Muktasari:

  • Mgombea urais wa Chaumma, Salum Mwalimu amesema akishinda nafasi hiyo atamwomba Tundu Lissu washirikiane kuleta mabadiliko nchini.

Karatu. Mtiania wa urais wa Tanzania wa Chaumma, Salum Mwalimu ameweka nia ya kushirikiana na Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu ikiwa atashinda urais.

Mwalimu ambaye yupo mkoani Arusha katika ziara ya kutafuta wadhamini, leo Ijumaa Agosti 22, 2025, amesema hana mgogoro na Tundu Lissu.

"Mimi sina kinyongo na Tundu Lissu, nikishinda uchaguzi huu, nitamwendea na kumwambia urais huu hapa kijana wako nimepambana nimeupata, tufanyeje kuleta mageuzi katika nchi yetu," amesema.

Mwalimu amesisitiza kuwa, Chaumma itakuwa tayali kushirikiana na Chadema bila kinyongo, akibainisha kuwa hakuondoka kwenye chama hicho kwa ugomvi.

Amesema, alifikia uamzi huo ili kupata chama kinachoshiriki uchaguzi baada ya chama chake cha zamani kuweka msimamo wa kutoshiriki uchaguzi huo bila kuwepo kwa mabadiliko ya sheria za uchaguzi.

Mwalimu ambaye pia ni katibu mkuu wa Chaumma, alijiunga na chama hicho Mei mwaka huu baada ya kujivua nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema - Zanzibar na kujivua uanachama wa chama hicho.

Yeye na wenzake waliokuwa viongozi waandamizi wa Chadema wakiwemo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Bara, Benson Kigaila na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema wote walijiunga na Chaumma.

Baada ya kujiunga Chaumma, Mwalimu aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho huku Benson Kigaila na John Mrema wakichukua nafasi kama za zamani.

Mgombea mwenza wa mtiania huyo, Devotha Minja, naye ni miongoni mwa waliojiunga Chaumma wakitokea Chadema, yeye alipojiunga na chama hicho aliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chaumma - Bara na mgombea mwenza wa kiti cha urais.