Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wazee Karatu wamkabidhi vazi, fimbo mtiania wa urais wa Chaumma Salum Mwalimu

Muktasari:

  • Mwalimu apokea vazi, kifimbo cha wazee wa kimila Karatu, dhamira ni kumlinda katika safari yake ya kwania katika nia yake ya kuteuliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuwania urais.

Karatu. Mtiania wa urais wa Tanzania wa Chaumma, Salum Mwalimu amepokea vazi na kifimbo kutoka kwa wazee wa kimila wilayani Karatu mkoani Manyara ikiwa ni ishara ya kumlinda katika safari yake ya kuwania urais.

Mtiania huyo, amekabidhiwa vielelezo hivyo vya jadi alipowasili wilayani humo kuzungumza na wakazi wa mji wa Karatu kuomba udhamini katika safari yake ya kugombea urais Tanzania.

"Tumemkabidhi fimbo hii kama ishara ya kumsimika imwepushe na mabaya katika safari yake," wamesema wazee hao.

Mwalimu amepokea zawadi hiyo na kuwashukuru wazee hao akiahidi kusonga mbele kutimiza maombi yao.

"Nimepokea kwa unyenyekevu sala zenu wazee wa Karatu, nitasimama kutimiza maombi yenu," amesema.

Mwalimu anaendelea na ziara yake leo, ikiwa ni siku ya saba tangu alipoanza Jumamosi Agosti 16, 2025 mkoani Lindi akizunguka mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Iringa, Morogoro na Dodoma kabla ya kuingia Mkoa wa Manyara.