Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwalimu aahidi kuendeleza maono ya Lowassa Monduli

Muktasari:

  • Mgombea urais wa Chaumma, Salum Mwalimu, amewaomba wananchi wa Monduli kumpigia kura ili kuendeleza maono ya hayati Edward Lowassa. Katika kampeni yake, amesisitiza kupambana na udhalimu na kushughulikia changamoto za ardhi, miundombinu, huduma muhimu na masoko.

Arusha. Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu, amewaomba wananchi wa Monduli kumpigia kura katika uchaguzi mkuu  Oktoba 29, 2025 ili aendeleze maono ya hayati Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri Mkuu na mbunge wa muda mrefu wa eneo hilo.

Lowassa, aliyefariki dunia Februari 10, 2024, alihudumu kama Mbunge wa Monduli kwa miaka mingi na alikuwa miongoni mwa wanasiasa wakongwe waliokuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Tanzania.

Akizungumza leo, Septemba 7, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika soko la wafanyabiashara wadogo la Jumapili, wilayani Monduli, mkoani Arusha, Mwalimu amesema kwamba Lowassa alikuwa kiongozi mwenye maono makubwa ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini na haipaswi kuruhusu maono hayo kufifia kwa kuwa hayupo tena.

"Ninawaomba watu wa Monduli mniamini. Najua shida mnazopitia kama wafugaji, naomba mniamini niyabebe yale maono aliyokuwa nayo Lowassa. Kikubwa nisaidieni niende Ikulu nikapambane na udhalimu uliopo ili wananchi waneemeke," amesema Mwalimu.

Mwalimu amesema kuwa, pamoja na changamoto za kisiasa zilizomkumba Lowassa, alibaki kuwa kiongozi wa mfano aliyepigania mabadiliko, hata alipohamia upinzani mwaka 2015 baada ya kutokubaliana na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Lowassa alipojiunga Chadema Julai 2015, alisema CCM haikumtendea haki katika kupitisha majina ya wagombea urais hivyo asingeweza kuendelea kubaki kwenye chama hicho.

"Lowassa alikuwa na maono makubwa. Ndiyo maana alipoona CCM inamzingua, alihamia upinzani…Sasa tusikubali maono yale yapotee," amesisitiza.

Katika mkutano huo, aligusia pia matatizo yanayowakumba wakazi wa Monduli ikiwemo migogoro ya ardhi ya malisho, miundombinu mibovu ya masoko na ukosefu wa huduma muhimu.

Ameahidi kuyashughulikia endapo atachaguliwa kuwa Rais Oktoba 29, 2025.

Kwa upande wake, Leah Kweka, mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chaumma, amesema akipewa nafasi ataweka kipaumbele katika kushughulikia changamoto ya maji, barabara na huduma bora za soko la Jumapili.

"Watu hawaogi na wengine wako hapa siku ya tatu hawajaoga. Nikichaguliwa, nitakwenda kuzungumzia hili bungeni ili jamii ipate huduma hii muhimu," amesema Kweka.

Aidha, ameahidi kupigania kuboreshwa kwa miundombinu ya soko, kujengwa kwa vyoo na kuhakikisha wafanyabiashara wanapata mazingira bora ya kufanya shughuli zao.