Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

WIKI YA MWANANCHI: Manara kuharibu au kupatia?

LEO AGOSTI 29 ndio siku ya mwisho ya Wiki ya Mwananchi ambayo itafanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, huku mambo makubwa yakiandaliwa na uongozi wa klabu.

Huu ni mwaka wa tatu tangu Yanga ilipoanzisha Wiki ya Mwananchi kama wenzao Simba wanavyofanya kila mwaka kuwa na Simba Day ambayo inatarajiwa kufanyika Septemba 19.

Mwanaspoti, gazeti makini na pendwa la michezo na burudani nchini linakuangazia matukio makubwa matano ambayo yatabamba leo.


MOTO WA KOFFI, NANDY

Gwiji wa kimataifa wa muziki wa lingala huko DR Congo, Koffi Olomide na staa wa kike anayetamba katika anga la muziki wa kizazi kipya nchini, Faustina Mfinanga maarufu ‘Nandy’ wataliamsha dude katika tamasha hilo, huku akitarajiwa kuimba wimbo maalumu kwa ajili ya siku hiyo.

Nandy mbali na kuimba wimbo maalumu ambao ameutengeneza mithili ya singeli ambayo ni habari ya mujini kwa sasa, pia atapata nafasi ya kuimba ngoma yake ya ‘Leo Leo’ aliyomshirikisha Koffi Olomide.

Vilevile siku hiyo anaweza kutoa sapraizi kubwa kwa Wananchi ikisemekana atapanda jukwaa moja na mchumba wake, Billinas ambaye pia ni Yanga kindakindaki.

Hakuna ubishi kuwa balaa la Koffi awapo jukwaani, hivyo Wiki ya Mwananchi mwaka huu inaonekana kufana kabla hata ya siku kufika. Mwaka jana Yanga walimwalika Harmonize kuwatumbuiza.

Wasanii wengine watakaopamba tamasha hilo ni G-Nako, Chegge, Mhe. Temba, Mzee wa Bwax, Baba Levo, Stamina, Madee, Sir Juma Nature, Shetta na wengineo.


UTAMBULISHO

Utambulisho unasubiriwa kwa hamu na Wanajangwani hao kutokana na namna ambavyo aliyekuwa msemaji wa Simba, Haji Manara atakavyomwaga vionjo.

Katika tamasha hilo mshereheshaji huwa ni mtangazaji nguli wa michezo nchini, Maulid Kitenge akisaidiana na mhamasishaji Antonio Nugaz, lakini awamu hii jukumu hilo limeandaliwa maalumu kwa Manara.

Hakuna asiyejua vibweka vya Manara, hivyo utambulisho hasa wa majina ya mastaa wa klabu hiyo utakuwa wa aina yake.


MANARA KUPATIA/KUHARIBU

Mbali na vitu vingi vitakavyojiri siku hiyo, lakini Manara anatazamiwa kuwa kivutio zaidi kwani atahitaji kufanya jambo kubwa zaidi ya alikotoka.

Hakuna anayepinga wala kutojua balaa la Manara pale anapokuwa anaamini kile anachokifanya, hivyo siku hiyo wengi wanasubiri kuona nini atakifanya kwa wana Jangwani ambao alikuwa akiwakebehi alipokuwa Msimbazi.

Lakini kutokana na namna ambavyo amepania siku hiyo, kuna mawili kuharibu au kupatia shughuli, maana anaonekana kupania.


NAMNA MASTAA WATAKAVYOTUA

Mwaka huu inasubiriwa kwa hamu zaidi namna mastaa mbalimbali watakavyotimba uwanjani baada ya mwaka jana Harmonize kushuka na kamba akitokea juu ya paa mpaka katikati ya uwanja.

Kutokana na tukio hilo, wana Yanga wengi wanasubiri sapraizi mwaka huu wakitakata kujua wataingia na nini, baada ya mwaka uliopita kutumia pia farasi huku wenzao Simba wakiingia na helkopta.


MASTAA KUTOKAJE?

Tamasha la mwaka jana lilinoga kwa mengi, kwani mastaa wote walivishwa suti kali na kuwapa burudani mashabiki kabla ya baadaye kutengeneza duara moja matata kabisa kisha kuzunguka uwanja mzima kuwasalimia mashabiki na wapenzi walioujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Msimu huu inawezakana kukaibuka mtoko mpya ambao utalinogesha tamasha hilo, mbali na burudani ya mechi mbalimbali kabla ya Wazambia - Zanaco kuvaana na wenyeji wao Yanga kuhitimisha kilele cha Wiki ya Mwananchi.