Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mmoja afariki mwingine akijeruhiwa ajali ya basi, lori Mbeya

Muktasari:

  • Ajali hiyo imetokea leo Ijumaa Aprili 25, 2025 katika eneo la Igawa wilayani Mbarali mkoani Mbeya likihusisha magari mawili na kuua na kujeruhi mmoja.

Mbeya. Mtu mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili mkoani Mbeya, huku Jeshi la Polisi likitoa tahadhari kwa madereva kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani.

Ajali hiyo imetokea leo Aprili 25, 2025 katika eneo la Igawa mkoani humo, likihusisha basi la kampuni ya Hai Express kuligonga lori Kampuni ya AM Motors ya Zambia.

Akithibitisha ajali hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi kutaka kuyapita magari mengine na kugongana uso kwa uso na lori hilo lililokuwa likitokea Zambia.

Amesema katika ajali hiyo, dereva wa basi hilo, Bosco Mwamila amefariki papo hapo, huku mwanafunzi Gadiel George (6) wa Shule ya Msingi Isaya akijeruhiwa na kuwahishwa Hospitali ya Wilaya ya Mbarali kwa matibabu.

"Chanzo ni uzembe wa dereva wa basi la Hai Express ambaye alitaka kuyapita magari mengine bila tahadhari na kuligonga Lori hilo lililokuwa likielekea Dar es Salaam kutokea Zambia," amesema Kuzaga.

Kamanda huyo ametoa rai kwa madereva kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani ili kuondokana na ajali zisizo za lazima akieleza kuwa jeshi hilo linaendelea kuchukua hatua kwa madereva wasiozingatia sheria barabarani ikiwamo kuwafungia leseni.

Mmoja wa mashuhuda na dereva wa lori, Ismail Seleman amesema muda mwingine madereva huwa chanzo cha ajali kwa kutofuata sheria na alama za barabarani.

"Bila kuzingatia mbele kuna nini, ameona mwenzake anatenbea kwa 50, yeye akaamua kupita ndio akakutana na lori hilo likapiga kuanzia kioo hadi kubana ubavuni kisha kukwepa," amesema shuhuda huyo.