Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wababe wa Simba, Yanga hadharani CAF

Muktasari:

  • Hii ina maana kwamba, baada ya hatua ya kwanza, timu 32 zitacheza hatua ya pili na kubakiza timu 16 ambazo zitaingia hatua ya makundi ambayo kila kundi litakuwa na timu nne.

Wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba na Yanga, wametangaziwa rasmi kuanza  michuano hiyo katika raundi ya kwanza, kufuatia mabadiliko makubwa yaliyofanywa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa msimu wa 2025/26.

Droo ya ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na ile ya Kombe la Shirikisho inatarajiwa kupangwa Dar es Salaam kesho, ikiwa ni mara ya kwanza inafanyika nje ya nchi ya Misri baada ya kupita miaka mingi.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya CAF, msimu huu utashuhudia klabu 62 zikishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini tofauti na miaka ya nyuma ambapo klabu nne hadi sita zilikuwa zinaanza moja kwa moja hatua ya pili, mwaka huu ni klabu mbili tu ambazo ni Al Ahly ya Misri na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ndiyo zitaanzia hatua hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ni kwamba timu 60 zitacheza hatua ya kwanza, ambapo 30 zitaungana na Mamelodi na Ahly katika hatua inayofuata na kuwa timu 32, hii ina maana kuwa sasa kuna uwezekano wa vigogo wakubwa wakatolewa kwenye hatua ya kwanza ya michuano hiyo kutoka na droo hiyo itakayofanyika kwa uwazi kutoka na wakubwa wengi kuungana huku.

Hivyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga pamoja na watani wao wa jadi Simba ambao watashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wote watalazimika kuanza kampeni yao ya CAF kuanzia raundi hii ambayo mechi zake za kwanza zitapigwa kuanzia Septemba 19, 2025.

Msimu uliopita Yanga ilianzia raundi hii pamoja na Azam FC, lakini huko nyuma Simba ilikuwa ikianzia raundi ya pili, ambapo ilikuwa ikicheza mechi moja ya nyumbani na ugenini na kutinga hatua ya makundi lakini sasa ni tofauti, italazimika kucheza na wapinzani wawili tofauti.

Hii ina maana kwamba, baada ya hatua ya kwanza, timu 32 zitacheza hatua ya pili na kubakiza timu 16 ambazo zitaingia hatua ya makundi ambayo kila kundi litakuwa na timu nne.

Uamuzi wa CAF kuileta droo hiyo Tanzania unatokana na mafanikio ya soka Afrika Mashariki na ongezeko kubwa la watazamaji kutoka ukanda huo, hasa kutokana na mchango wa klabu kama Simba na Yanga kwenye mashindano ya kimataifa, lakini pia uwepo wa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani CHAN ambayo yanaendelea kwa sasa yakishirikisha mataifa 19, kwenye nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Azam Media, ambao ni washirika wa kimkakati wa CAF kwa ukanda wa Afrika Mashariki, wamepewa heshima ya kuandaa droo hiyo baada ya mafanikio ya matukio kama haya kwenye studio za SuperSport na beIN Sports.

Droo hiyo itaonyeshwa mubashara kupitia YouTube ya CAF na vituo vingine vya matangazo. Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho itaanza rasmi Novemba 21, 2025, huku hatua ya mtoano ikipangwa kuanza Machi 13, 2026.

Wakati Simba na Yanga wakianza mapema, wawakilishi wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika Azam FC na Singida Black Stars nao watalazimika kupitia mlango huohuo wa hatua ya awali, lakini huku timu sita hazitacheza hatua hii.

Timu za Zamalek, Wydad Casablanca, USM Alger, CR Belouizidad Al Masry na Stellebosch zitaanzia hatua ya pili ya michuano hiyo ambayo inashirikisha jumla ya timu 58 kutoka barani Afrika.