Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waamuzi Waarabu wapewa Dabi ya Kariakoo

Muktasari:

  • Hii inakuwa mara ya kwanza kihistoria kwa mchezo huo kuamuliwa na waamuzi kutoka nje wakati timu hizo mbili kubwa mbili zinapokutana kwenye mashindano ya ndani.

Mchezo wa Dabi ya Kariakoo umeingia kwenye historia mpya baada ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kuwashusha waamuzi kutoka Uarabuni kuamua mchezo huo.

Taarifa iliyotolewa na bodi hiyo muda mfupi uliopita ni kwamba mchezo huo utaamuliwa na mwamuzi Amin Omar atakayekuwa mwamuzi wa kati, akisaidiwa na Mahmoud El Regal, Samir Mohamed wakati mwamuzi wa nne mezani akiwa Ahmed Elghandour wote kutoka Misri huku mtathimini waamuzi akipewa Alli Mohamed kutoka Somalia.

Hii inakuwa mara ya kwanza kihistoria kwa mchezo huo kuamuliwa na waamuzi kutokanje wakati timu hizo kubwa mbili zinapokutana kwenye mashindano ya ndani.

Rekodi zinaonyesha Omar amewahi kusimamia mechi mbili za mashindano ya Afrika kwa timu hizo mbili, ambazo zote hakuna timu iliyoshinda.

Omar alisimamia mchezo wa nyumbani wa Yanga dhidi ya Mamelodi msimu uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika, mechi ikimalizika wa sare isiyo na mabao.

Mwamuzi huyo pia aliamua mchezo wa Horoya dhidi ya Simba, ambapo wekundu hao walilala kwa bao 1-0 ikiwa pia ni mechi ya Ligi ya mabingwa.

Awali TPLB kabla ya mchezo huo kuahirishwa mara mbili ulipangwa kuchezeshwa na waamuzi Watanzania akiwemo Ahmed Arajiga lakini sasa wakabadilishwa baada ya Arajiga kwenda kwenye kozi.

Omar sio mwamuzi rahisi akiwa uwanjani ambapo ana rekodi ya kumwaga kadi nyingi za njano na nyekundu ambapo suala la kuamua penalti sio suala gumu kwake.

Rekodi zake zinaonyesha kuwa amefanikiwa kuchezesha michezo 239, akitoa kadi za njano 823 na nyekundu 20 huku akitoa penalti 85 kwenye michezo yote.