Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UEFA yalegeza kanuni ya usajili ikizisubirisha La Liga, Serie A

Muktasari:

  • Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu huu wa 2025/2026 itafanyika Mei 30, 2026 katika Uwanja wa Puskas Arena, Hungary.

Umoja wa Vyama vya Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) umelainisha kanuni yake ya usajili kwa timu zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya, uamuzi ambao unaweza kupokelewa kwa hisia chanya na klabu shiriki.

Kanuni hiyo ni ile ya kulazimisha kila timu kuwa na kikosi cha wachezaji 25 tu kutumika katika hatua ya ligi ya mashindano hayo.

Hilo limepelekea timu kuweka kando baadhi ya mastaa wao katika sajili ambazo zimewasilisha kwa UEFA na fursa pekee iliyokuwepo kwa nyota hao ni kucheza hatua ya mtoano iwapo timu hizo zitafanikiwa kuingia.

Lakini hata hivyo UEFA imelegeza kwa kuongeza kipengele cha kuruhusu klabu kuingiza jina la mchezaji wakati hatua ya ligi ikichezwa iwapo kutakuwa na mchezaji katika kikosi cha watu 25 kilichosajiliwa, atapata majeraha au ugonjwa utakaomfanya akae nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Kanuni hiyo itatumika hadi katika mechi ya sita ya hatua ya ligi ya mashindano hayo katika muda ambao hatua ya makundi ya mashindano ya Conference League itakuwa inafikia tamati.

Taarifa iliyotolewa na UEFA imeleeza kwamba uamuzi huo unalenga kulinda wachezaji.

“Fikra ya kuendana na hili ni kuhakikisha waliopo katika orodha ya kikosi hawapunguzwi kwa kutozingatia usawa na wachezaji wanalindwa dhidi ya presha ya kutumika sana,” imefafanua taarifa ya UEFA.

Ikumbukwe baadhi ya nyota wamejikuta wakiwekwa kando katika usajili wa klabu zao kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu ili kukidhi matakwa ya kanuni hiyo.

Mfano Arsenal ililazimika kuweka kando jina la Gabriel Jesus, Tottenham Hotspur ikifanya hivyo kwa Mathys Tel, Chelsea ikimuweka kando Facundo Buononotte na Federico Chiesa akiwa muhanga upande wa Liverpool.

Katika hatua nyingine, UEFA imeamua kujiongezea muda wa kufanya tathmini kabla haijatoa majibu ya maombi ya Ligi Kuu za Hispania ‘La Liga’ na Italia ‘Serie A’ za kutaka baadhi ya mechi zao kuchezwa nje ya bara la Ulaya.

Hiyo inakuja kufuatia ombi la La Liga la kutaka mechi baina ya Barcelona na Villarreal kuchezwa Marekani mwezi Desemba mwaka huu huku Serie ikiomba mchezo baina ya AC Milan na Como kuchezwa Australia, Februari mwakani.

“Kamati (ya Utendaji) inatambua umuhimu wa hili kama jambo linalokua lakini inafafanua hamu ya kuhakikisha kwamba lina maoni ya wadau wote kabla ya kuja na uamuzi wa mwisho,” imefafanua taarifa ya UEFA.