Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal kupangiwa vigogo hawa Ligi ya Mabingwa Ulaya

UEFA Pict

Muktasari:

  • Kinachoelezwa ni kwamba Arsenal moja ya mechi zake inaweza kupangiwa ugenini kwenda kukabiliana na mabingwa mara 15, Real Madrid, mechi ambayo miamba hiyo ya Bernabeu inaweza kuhitaji kulipa kisasi baada ya kutupwa nje hatua ya robo fainali na Arsenal msimu uliopita.

Monaco, Ufaransa. Droo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itapangwa leo Alhamisi, Agosti 28, huku Arsenal ikiripotiwa kuwa hatarini kupangiwa timu ngumu.

Droo hiyo imepangwa kufanyika huko Monaco, Ufaransa. Na sasa kocha Mikel Arteta anaomba timu yake isiwekwe kwenye kundi la kukutana na timu ngumu katika mtindo mpya wa michuano hiyo.

Kinachoelezwa ni kwamba Arsenal moja ya mechi zake inaweza kupangiwa ugenini kwenda kukabiliana na mabingwa mara 15, Real Madrid, mechi ambayo miamba hiyo ya Bernabeu inaweza kuhitaji kulipa kisasi baada ya kutupwa nje hatua ya robo fainali na Arsenal msimu uliopita.

UEF 01

Mechi hiyo inaweza kufuatiwa na washindi wa pili wa msimu uliopita, Inter Milan. Lakini, pia Arsenal inaweza kukabiliwa na mechi nyingine ngumu dhidi ya Atletico Madrid, Napoli na timu ya Ubelgiji, Royale Union Saint-Gilloise.

Hata hivyo, Arsenal si timu pekee ya England iliyo kwenye hatari ya kupangiwa ratiba ngumu kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambayo itachezwa kwa mtindo wa ligi, lakini kila timu ikiwa na mechi zake.

UEF 02

Chelsea inaweza kuanza kampeni kwa kukabiliana na Bayern Munich na Barcelona. The Blues inaweza pia kwenda Kazakhstan kuwakabili FC Kairat, ambao wameitupa nje Celtic kwenye mechi za mchujo za kufuzu michuano hiyo.

UEF 06
UEF 06

Liverpool ina matumaini makubwa ya kupata bahati kwenye upangaji wa droo huyo. Kikosi hicho cha kocha Arne Slot kilimaliza vinara wa michuano hiyo kwenye hatua ya makundi baada ya kushinda mechi saba kati ya nane.

UEF 03

Msimu huu, miamba hiyo ya Anfield inaweza kupangwa kuwakabili Borussia Dortmund, Madrid, Ajax na AS Monaco, huku Manchester City inaweza kupangwa kuzikabili Inter, Bayern, Bayer Leverkusen na Atletico Madrid.

UEF 04

Tottenham iliyofuzu kwa kupitia ushindi kwenye fainali ya Europa League dhidi ya Manchester United itakuwa na balaa pia, ambapo inaweza kupangwa kucheza na Barcelona na mabingwa watetezi, Paris Saint-Germain.

UEF 05

Hiyo ni kwenye hatua ya makundi ambayo itacheza kwa mtindo wa ligi moja, ambapo kila timu itacheza mechi nane ili kupata tiketi ya kufuzu mtoano.