Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ten Hag yupo sana Man United

Manchester, England. Kwa wale waliokuwa wanasubiri kocha wa Manchester United Erik ten Hag aondoke kwenye timu hiyo, watasubiri sana.

Mashabiki wengi wa Manchester United wamekuwa hawamtaki kocha huyo baada ya timu hiyo kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu England kwa kipindi cha hivi karibuni.

Lakini taarifa ya jana imesema kuwa sasa kocha huyo ataendelea kubaki Manchester United kwa msimu ujao.

Hata hivyo, inafahamika kuwa United imefikia uamuzi huo baada ya kutafuta makocha kadhaa wakubwa wakagoma kujiunga na timu hiyo, lakini wengine wakishinikiza usajili mkubwa kufanyika.

Sasa mabosi wa United wanajiandaa kujadili mkataba mpya na kocha huyo ambaye ameonekana akiwa mapumzikoni Ibiza anakula bata.

Hata hivyo, chanzo kinasema kuwa mabosi wa United wamesema baada ya kocha huyo kutwaa ubingwa wa Kombe la FA alijiongezea thamani ya kubaki kwenye timu hiyo kwa kuwa ni moja ya tageti ambayo walikuwa wamempa.

Makocha walikuwa wanazungumza na mabosi wa United ili waridhi kiti hicho ni Mauricio Pochettino, Thomas Tuchel na  Thomas Frank lakini wote inaelezwa walimgomea bosi wa United  Sir Jim Ratcliffe.

Hata hivyo, kocha wa mwisho kukutana na bosi huyo alikuwa  Tuchel ambaye walikaa pamoja kwa ajili ya chakula cha usiku nchini Ufaransa, lakini kocha huyo alimweleza bosi huyo kuwa hawezi kujiunga na United kwa sasa.

Taarifa zinasema kuwa United wapo tayari kumpa sapoti ya kutosha Ten Hag ili kuhakikisha kuwa timu hiyo inapata mafanikio kwa ajili ya msimu ujao, huku tageti namba moja ikiwa kuirudisha kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hii ina maana kuwa baadaye mwezi ujao, Ten Hag atarejea United kwa ajili ya kwenda na timu hiyo kwenye maandalizi ya msimu mpya wa ligi.
Taarifa zinasema kuwa kocha huyo alishaacha pendekezo la majina ya usajili yanayotakiwa kwenye timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.

Mastaa wapya wataungana na Andre Onana, Rasmus Hojlund,  Kobbie Mainoo na Alejandro Garnacho ambao walionyesha kiwango cha juu msimu uliopita. 

Omar Berrada anatarajiwa kuwa mtendaji mpya wa United kuanzia Julai 13 akiwa anatoka Manchester City lakini pia timu hiyo inataka kumuongeza kwenye bodi ya wakurugenzi  Dan Ashworth  kutokana Newcastle.