Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Yanga zapanda viwango vya ubora CAF

Muktasari:

  • Viwango vya ubora wa klabu vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) hupimwa kwa kuangalia mafanikio ya ushiriki wa timu katika mashindano ya klabu Afrika kwa kipindi cha miaka mitano.

Dar es Salaam. Simba imeendelea kuonyesha ukubwa wake Afrika baada ya kupaa katika viwango vya ubora wa klabu vya CAF hadi nafasi ya tano huku mtani wake Yanga naye akipanda.

Kwa Simba kuwa nafasi ya tano inamaanisha imepanda kwa nafasi mbili kutoka ya saba ambayo ilikuwepo kabla ya kuanza msimu uliopita.

Kwa mujibu wa chati ya CAF iliyotolewa leo, Simba ipo nafasi ya tano kutokana na pointi zake 48 ilizokusanya katika ushiriki wake kwenye mashindano ya klabu ya Shirikisho hilo katika misimu mitano iliyopita.

Wakati Simba ikiwa na pointi 48, Yanga ipo nafasi ya 12 kutokana na pointi zake 34 ambazo imekusanya katika kipindi hicho.

Kuwepo nafasi ya 12 kunamaanisha Yanga imesogea kwa nafasi moja kutoka nafasi ya 13 ambayo ilikuwepo katika chati ya mwaka jana.

Chati hiyo ya CAF ndio itatumika katika kuchezesha droo ya mashindano ya Klabu Afrika kwa msimu ujao ambayo imepangwa kufanyika kesho Jumamosi, Agosti 9, 2025 jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Katika kipindi cha misimu mitano iliyopita, Simba imefika hatua ya fainali Mara moja huku mara nne ikiishia robo fainali. Yanga ndani ya kipindi hicho imefika fainali mara moja, robo fainali mara moja na hatua ya makundi mara moja.

Orodha hiyo ya klabu bora Afrika inaongozwa na Al Ahly ikifuatiwa na Mamelodi Sundowns huku Esperance ikiwa nafasi ya tatu.

Nafasi ya nne ipo RS Berkane, Simba ya tano, Pyramids FC ipo katika nafasi ya sita na timu iliyopo katika nafasi ya saba ni Zamalek. Wydad ipo nafasi ya nane ikifuatiwa na USM Alger, nafasi ya kumi kuna CR Belouizdad.

Droo ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika itachezeshwa kesho Mchana jijini Dar es Salaam.

Ni timu mbili tu ambazo hazitoanzia katika hatua ya kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo ni Al Ahly ya Misri na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Timu hizo zote mbili hivi karibuni ziliiwakilisha Afrika katika Fainali za Kombe la Dunia la Klabu zilizofanyika Marekani na Chelsea ikaibuka bingwa.

Ukiondoa hizo, timu nyingine mbili zilizoiwakilisha Afrika zilikuwa ni Esperance ya Tunisia na Wydad AC ya Morocco.