Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Berkane zapishana dakika nne

Pikipiki kubwa aina ya Kawasaki, ikiwa imebeba askari mwenye miwani meusi, ilionekana ikisonga kwa kasi katika viunga vya Uwanja wa Amaan, ikiashiria kuwasili kwa msafara wa timu ya Simba SC kwa ajili ya mechi ya  marudiano ya fainali ya pili dhidi ya RS Berkane.

Basi la Simba, lenye utambulisho wa jina la timu hiyo, liliingia kwa kasi ya wastani ndani ya uwanja huo saa 8:21 mchana. Ndani, wachezaji walionekana wakitazama dirishani huku wengine wakiwa wamevalia headphones.

Baada ya basi kusimama, mmoja baada ya mwingine walianza kushuka. Kipa Moussa Camara alishuka, akiwa na uso wa kujiamini, akifuatiwa na wachezaji wengine akiwemo beki Che Malone Fondoh.

Charles Jean Ahoua, Ellie Mpanzu na wachezaji wengine walishuka na moja kwa moja kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo.

Maofisa wa CAF walihakikisha kila kitu kipo sawa, huku viongozi wa Simba wakisimama pembeni kutoa maelekezo ya mwisho.

Dakika nne baadaye, saa 8:25, king’ora kingine kilisikika safari hii kikitangaza ujio wa RS Berkane. Msafara wao uliingia kwa utulivu lakini wenye hadhi kubwa, wakisindikizwa na magari mawili ya polisi na moja la usalama wa timu hiyo.

Tofauti na Simba ambao walishuka kwa hisia tofaufi za nyumbani, Berkane walionekana na sura za upole wa ukimya na kutembea kwa utulivu hadi vyumba vya kubadilishia nguo.