Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM Ruangwa: Majaliwa hatogombea tena ubunge

Muktasari:

  • Majaliwa amekuwa mbunge wa Ruangwa kwa miaka 15 mfululizo kuanzia mwaka 2010. Aliapishwa kuwa Waziri Mkuu, Novemba 16, 2020 na Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, hayati Joseph Magufuli.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa hatogombea tena ubunge wa Ruangwa, Mkoa wa Lindi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025.

Dirisha la uchukuaji na urejeshaji fomu CCM za udiwani na ubunge lilifunguliwa kuanzia Juni 28, 2025 na linafungwa saa 10:00 jioni ya leo Jumatano, Julai 2025.

Uamuzi wa Majaliwa umetangazwa leo Jumatano na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ruangwa, Mkoa wa Lindi, Abbas Makwetta ambaye amesema:“Mheshimiwa Majaliwa amekuja na kusema hagombei tena ubunge.”

Majaliwa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Tanzania amekuwa Mbunge wa Ruangwa kwa miaka 15 mfululizo kuanzia mwaka 2010. Katika utawala wa awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, ndipo aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Julai 2, 2025, Makwetta amesema: “Mheshimiwa Waziri Mkuu amekuja hapa leo saa 4 asubuhi na hakuja kuchukua fomu ila amekuja kusema hatogombea.”

“Amesema amelitumikia jimbo kwa kipindi cha miaka 15, ametafakari na kuamua waachie vijana ili waendelee na hatua zingine. Lakini amewataka wana Ruangwa kuhakikisha Samia, Mwinyi wanapata kura za kutosha.”

Hata hivyo, mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kutoka kwa Majaliwa mwenyewe ama ofisi yake kuhusiana na uamuzi huo.

Katibu huyo wa CCM amesema hadi saa 5 asubuhi ya leo Jumatano Julai 2, waliojitokeza kuchukua fomu kuomba ridhaa ya kuwania jimbo hilo ni watano.

Juni 26, 2025 akitoa hotuba yake katika mkutano wa Bunge jijini Dodoma, Majaliwa pamoja na mambo mengine aliwashukuru wana Ruangwa kwa kumpa ushirikiano mkubwa katika kipindi chote akiwa mbunge wao.

“Naomba Mwenyezi Mungu azidi kuimarisha mshikamano tulionao na naomba kuwajulisha nakuja kuchukua fomu na kuomba tena ridhaa yenu,” alisema Majaliwa huku akishangiliwa na wabunge. 

Majaliwa anahitimisha safari ya ubunge na uwaziri mkuu akiwa na miaka 64. Alizaliwa Desemba 22, 1960 katika Kijiji cha Mnacho, Wilaya ya Ruangwa. Kitaalamu, Majaliwa ni mwalimu