Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais CAF aunga mkono Senegal kukata rufaa

Muktasari:

  • Senegal imetangaza kukata rufaa katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) iliyoko Lausanne, Uswisi, kwa lengo la kutafuta haki ya mwisho katika sakata hilo.

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe, ametoa msimamo wake kuhusu uamuzi wa Bodi ya Rufaa ya CAF kuwapoka Senegal ubingwa wa AFCON 2025 na kuwapa Morocco.

Kauli ya Motsepe imekuja baada ya Bodi ya Rufaa ya CAF, usiku wa Machi 18, 2025 kutangaza kwamba, Morocco imeshinda rufaa yake, hivyo imebatilisha matokeo ya kipigo chao cha bao 1-0 kwenye fainali dhidi ya Senegal kufuatia tukio la utata la kutoka uwanjani.

Baada ya uamuzi huo, kumekuwa na mjadala mkubwa ambapo wapo wanaounga mkono, huku wengine wakipingana na suala hilo wakisema Senegal inanyimwa haki yao kutokana na kushinda ndani ya uwanja.

Akizungumzia sakata hilo, Motsepe amesema: "Nimefahamishwa juu ya uamuzi wa Bodi ya Rufaa ya CAF kuhusiana na rufaa ya Morocco kuhusu mechi ya fainali ya AFCON Morocco 2025, na hapo awali nilieleza kutoridhishwa kwangu kwa kiwango kikubwa kuhusu matukio yaliyotokea katika mechi hiyo ya fainali.

"Jambo muhimu kuhusu yaliyotokea katika mechi hiyo ya fainali ni kwamba yalidhoofisha kazi nzuri ambayo CAF imekuwa ikifanya kwa miaka mingi kuhakikisha kuna uadilifu, heshima, maadili, utawala bora pamoja na uaminifu wa matokeo ya mechi zetu za mpira wa miguu."

Motsepe ameongeza kuwa: "Matukio yale yaliyotokea katika fainali ya AFCON Morocco yanaendelea kuchochea hali ya mashaka na kutokuaminiana ambayo bado tunakabiliana nayo.

"Hili ni tatizo la muda mrefu. Nilipoingia madarakani kama rais, moja ya changamoto kubwa ilikuwa ni kuhakikisha kutokuwepo upendeleo, uhuru na heshima kwa waamuzi na makamishna wa mechi.

"Kazi kubwa na nzuri imefanyika. Lakini bado kuna mashaka yanayoendelea kwa sababu hili ni tatizo la muda mrefu ambalo limekuwepo kwa miaka mingi, na tunaendelea kulishughulikia kwa sababu ni jambo la msingi sana."

Rais huyo ameendelea kwa kusema: "Suala jingine muhimu ambalo matukio ya fainali hiyo yameibua ni uhuru na heshima ya vyombo vyetu vya kimahakama. Katika kuchagua wajumbe wa vyombo hivyo, tulifuata njia tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

"Tulialika kila chama mwanachama na kila kanda kati ya kanda sita za CAF kupendekeza majina ya majaji na mawakili wanaoheshimika, kwa sababu ni muhimu uamuzi wa Bodi ya Nidhamu ya CAF na Bodi ya Rufaa ya CAF uheshimiwe na kuonekana kuwa na uadilifu.

"Ukichunguza muundo wa vyombo hivyo, utaona unajumuisha baadhi ya mawakili na majaji wanaoheshimika zaidi barani Afrika. Hata hivyo, bado tutalazimika kushughulikia mitazamo na wasiwasi kuhusu uadilifu. Hili ni suala endelevu.

"Sisi CAF tumejizatiti kuhakikisha kwamba si tu katika vitendo vyetu, bali pia tumetekeleza viwango bora. Tumewateua majaji na mawakili kutoka kila kanda na kila nchi kati ya 54 za Afrika kuhakikisha ni watu wenye uadilifu na historia nzuri ya kazi.

"Sehemu ya kuonyesha uhuru huo inaonekana katika uamuzi uliotolewa na vyombo viwili: Bodi ya Nidhamu ya CAF ilitoa uamuzi mmoja, na Bodi ya Rufaa ya CAF ikachukua msimamo tofauti kabisa."

Kuhusu taarifa za Senegal kujipanga kukata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (CAS), Motsepe ameunga mkono hilo akisema: "Nimefahamishwa pia kwamba Senegal inatarajia kukata rufaa, jambo ambalo ni muhimu.

"Kila moja ya nchi 54 za Afrika ina haki ya kufuatilia rufaa zao na kulinda maslahi yao, si tu ndani ya CAF bali pia katika chombo cha juu zaidi, ambacho ni CAS. Na sisi tutaheshimu uamuzi utakaotolewa katika ngazi hiyo ya juu. Jambo la msingi ni kwamba hakuna nchi hata moja barani Afrika itakayopewa upendeleo au faida ya kipekee kuliko nyingine.

"Tunachukulia kwa uzito mkubwa yaliyotokea katika mechi ya fainali ya AFCON Morocco 2025, na tayari tumeanza kuchukua hatua muhimu kuhakikisha maeneo yaliyobainika kuwa na upungufu yanaboreshwa kwa kupitisha maamuzi sahihi.

"Tumejiwekea viwango vya juu sana. Ni muhimu kwa mashabiki wa kawaida wa mpira wa miguu katika nchi zote 54 za Afrika, kwa mtazamo wao wenyewe, sio mtazamo wa CAF wala wangu kuona kwamba uamuzi wa vyombo vyetu vya kimahakama ni wa haki, wenye uadilifu na hauna upendeleo.

"Vilevile ni muhimu waamini kwamba waamuzi, waendeshaji wa VAR, na makamishna wa mechi ni watu wa haki na kwamba uamuzi wao unaonyesha uhuru na kutokuwepo kwa upendeleo, jambo ambalo ni muhimu sana."