Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CAF yaivua Senegal Ubingwa wa AFCON 2025, yaipa Morocco

Muktasari:

  • Fainali hiyo iliyochezwa Jumapili, Januari 18, 2025 iliingia doa katika dakika za majeruhi za muda wa kawaida wa mchezaji baada ya kundi kubwa la wachezaji na maofisa wa benchi la ufundi la Senegal wakiongozwa na Kocha Thiaw kugoma kwa muda kabla ya baadaye kuamua kuendelea na mechi.

Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) jana Jumanne, Machi 17, 2026 kwamba, kwa mujibu wa Kifungu cha 84 cha Kanuni za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), Timu ya Taifa ya Senegal imepoteza mechi ya fainali ya fainali hizo iliyochezwa Januari 18, 2026 na matokeo ya mechi hiyo  kuwa ushindi wa mabao 3–0 kwa Morocco.

Uamuzi huo unafuatia rufaa iliyowasilishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Morocco (FRMF) kuhusu utekelezaji wa vifungu vya 82 na 84 vya Kanuni za AFCON.

Kamati ya Rufaa ya CAF imetoa majibu na ufafanuzi wa baadhi ya hoja za rufaa hiyo.

Rufaa iliyowasilishwa na FRMF imekubalika kisheria na uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ya CAF umebatilishwa.

Kamati ya Rufaa ya CAF pia imebaini kuwa mwenendo wa timu ya Senegal unaangukia ndani ya wigo wa vifungu vya 82 na 84 vya Kanuni za AFCON.


Pingamizi lililowasilishwa na FRMF limekubaliwa.

Imetangazwa kuwa Senegal (FSF), imekiuka Kifungu cha 82 cha Kanuni za AFCON. Kwa mujibu wa Kifungu cha 84 cha Kanuni za AFCON, timu ya Senegal imetangazwa kupoteza mechi, na matokeo kurekodiwa kuwa 3–0 kwa faida ya Morocco.

Maombi yote mengine au madai ya nafuu yamekataliwa.”

Bodi ya Rufaa ya CAF pia imeamua kwamba, rufaa iliyowasilishwa kuhusu mchezaji Ismaël Saibari imekubaliwa kwa sehemu.

Bodi ya Rufaa ya CAF imethibitisha kuwa Bw. Ismaël Saibari alifanya utovu wa nidhamu kinyume na vifungu vya 82 na 83(1) kwa Kanuni za Nidhamu za CAF.

Adhabu iliyotolewa kwa Ismaël Saibari imebadilishwa kuwa kusimamishwa kushiriki mechi mbili rasmi za CAF, ambapo mechi moja imesimamishwa.

Faini ya dola za Kimarekani 100,000 (Sh261 milioni) iliyotolewa kwa Ismaël Saibari imefutwa.

Rufaa kuhusu tukio la wavulana wa kuokota mipira imekubaliwa kwa sehemu. Kamati ya Rufaa ya CAF imethibitisha kuwa FRMF inawajibika kwa mwenendo wa wavulana wa kuokota mipira wakati wa mechi husika.

Faini iliyotolewa kwa Morocco kuhusiana na tukio la wavulana wa kuokota mipira imepunguzwa hadi dola za Kimarekani 50,000 (Sh130 milioni). Rufaa kuhusu kuingiliwa kwa eneo la mapitio ya OFR/VAR imekataliwa.

Faini ya dola za Kimarekani 100,000 (Sh261 milioni) iliyotolewa kwa Morocco kuhusiana na tukio hilo imethibitishwa. Rufaa kuhusu tukio la kutumia leza imekubaliwa kwa sehemu.

Faini iliyotolewa kwa FRMF kuhusiana na tukio la leza imepunguzwa hadi dola za Kimarekani 10,000 (Sh26 milioni).

Fainali hiyo iliyochezwa Jumapili, Januari 18, 2025 iliingia doa katika dakika za majeruhi za muda wa kawaida wa mchezaji baada ya kundi kubwa la wachezaji na maofisa wa benchi la ufundi la Senegal wakiongozwa na Kocha Thiaw kugoma kwa muda kabla ya baadaye kuamua kuendelea na mechi.

Thiaw aliwaamuru wachezaji wake kutoka nje ya uwanja kufuatia uamuzi wa Refa Jean-Jacques Ndala, kuamuru penalti kwenda langoni mwao baada ya Brahim Diaz kufanyiwa faulo na Malick Diouf.

Hata hivyo nyota wa Senegal, Sadio Mane alionekana kutokubaliana na uamuzi wa kuondoka uwanjani ambapo alionekana akiwashawishi wenzake kuendelea na mchezo.

Uamuzi wa Senegal kurejea uwanjani na kuendelea na mchezo, ulikuwa na faida kwa upande wao kwani Morocco walikosa mkwaju huo wa penalti uliopigwa na Diaz na baadaye ikatwaa ubingwa kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Pape Gueye.