Mmoja afariki dunia, 30 walazwa

Muktasari:

  • Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 amefariki dunia baada ya msongamano uliokuwepo katika mchezo wa fainali iliyochezwa Uwanja wa Mkapa.

Dar es Salaam. Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametibitisha kutokea kifo cha mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 na wengine 30 kujeruhiwa baada ya msongamano katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Msongamano huo umetokana na wingi wa watu waliohudhuria uwanjani hapo kwa ajili ya kutazama mchezo wa fainali ya Kobe la Shirikisho baina ya Yanga dhidi ya USM Alger.

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili Mei 28, 2023 na Waziri Ummy kupitia mitandao yake ya kijamii imesema katika hali iliyotokea Uwanja wa Mkapa baada ya mashabiki kusongamana nje ya mageti na mengine kuvunjwa na mashabiki kuingia kwa nguvu uwanjani.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametibitisha kutokea kifo cha mtu mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 na wengine 30 kujeruhiwa baada ya msongamano katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Taarifa ya Awali: Kuhusu Majeruhi Mkapa Stadium Dar es Salaam. Hadi sasa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke imepokea majeruhi 30 ambapo 1 amefariki (Mwanaume mwenye umri wa takribani miaka 40.

Majeruhi wengi wanaendelea vizuri wana majereha madogomadogo, wanaendelea na vipimo.

Aidha timu kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ipo uwanjani, inafuatilia kwa karibu kuangalia kama kuna majeruhi wengine,” amesma Ummy.

Katika mchezo huo wa fainali ya kwanza Yanga imepoteza kwa mabao 2-1 huku timu hizo zikitarajiwa kucheza mechi ya marudiano Juni 3, mwaka huu.