Watanzania wafurika kwa Mkapa kushuhudia historia mkpya

Muktasari:

  • Yanga inatafuta historia nyingine katika soka la Afrika baada ya kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo itawavaa USM Alger.

Dar es Salaam. Wananchi wameitika ndicho unachoweza kusema ikiwa zimesalia saa chache kabla ya Yanga kucheza mchezo wao wa fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.

Wababe hao watakutana katika fainali hiyo ya kwanza itakayoanza muda mfupi ujao katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambao unaonekana kujaa mashabiki wa soka kushuhudia historia mpya Tanzania.

Uwanja wa Mkapa umetawala rangi za kijani, nyeusi na njano ambazo zinaonekana kutawala kwa Mkapa, Wananchi wanaonekana kuwa tayari kushuhudia timu yao ikiandika historia.

Ni maeneo machache ambayo yanaonekana kuwa wazi na kwa dalili zinavyoonekana kulingana na idadi ya mashabiki ambao wapo nje ni wazi kuwa uwanjani utajaa dakika chache zijazo.

Hakika huu ni mchezo wa fainali, Wananchi wapo na furaha huku vikundi mbalimbali vya ushangiliaji vikionekana kuanza kazi mapema.

Tayari kocha wa viungo wa Yanga na wa makipa wapo kwenye eneo la kuchezea ili kuweka mambo sawa kabla ya nyota wa timu hiyo kuingia uwanjani kupasha misuli na mazoezi madogo madogo kabla ya mchezo kuanza.