Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi aingia kwenye mtego mgumu PSG

Muktasari:

  • PARIS, UFARANSA. STAA mpya wa Klabu ya Paris Saint Germain, Muajentina Lionel Messi, amejikuta akiingia ndani ya mtego mgumu mara baada ya kusaini dili jipya la kuitumikia timu hiyo ambayo ina mjumuiko wa mastaa wengi wenye majina makubwa duniani.

PARIS, UFARANSA. STAA mpya wa Klabu ya Paris Saint Germain, Muajentina Lionel Messi, amejikuta akiingia ndani ya mtego mgumu mara baada ya kusaini dili jipya la kuitumikia timu hiyo ambayo ina mjumuiko wa mastaa wengi wenye majina makubwa duniani.

Messi amejiingiza kwenye mtego ambao utamfanya afanye kazi ya ziada ili aweze kujinasua. Tayari Messi amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia PSG, huku mkataba huo ukiwa na thamani ya Pauni 35 milioni kwa mwaka. Staa huyo atavuna pesa nyingi, lakini ukweli ana kazi kubwa ya kuhakikisha anavunja rekodi zilizopo ndani ya timu hiyo ili kutengeneza ufalme wake kama ilivyokuwa Barcelona.

Katika miaka 21 ya Messi ndani ya Barcelona amecheza michezo 778, kufunga mabao 672 na kuasisti 288.

Lakini kwa PSG maisha yatakuwa tofauti kwa sababu tayari kuna nyota wengine ambao wameweka rekodi nzuri za kupachika mabao na itamlazimu Messi kudhihirisha ubora ili aweze kumaliza utata huo.

Hiini orodha ya wachezaji wenye mabao mengi waliopo na waliowahi kupita PSG ambao anatakiwa kuwafunika ili ajinasue katika mtego huo.

Messi aingia kwenye mtego mgumu PSG

5. Angel Di MarÌa, mabao 88

Winga huyu alijiunga na PSG Agosti 6, 2015 akitokea Manchester United na hadi sasa ameichezea PSG michezo 264 na kufunga mabao 88. Katika msimu wa kwanza wa Di Maria akiwa na PSG alifanikiwa kuwa ndiye mchezaji aliyetoa pasi nyingi za mabao katika Ligi Kuu ya Ufaransa.

Msimu huo wa 2015/2016 alifunga mabao 14, ingawa msimu wa 2016/2017 hakuwa na wakati mzuri kwenye rekodi ya upachikaji mabao kutokana na kukosa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza, lakini pia alifunga mabao nane na kutoa asisti sita katika michezo 25 aliyocheza ambapo mara nyingi alikuwa akitokea benchi. Hii nayo ni miongoni mwa rekodi ambazo Messi atakuwa akiiwaza.

4. Pauleta, mabao 109

Mreno huyo alisainiwa na PSG akiwa na umri wa miaka 16 mara baada ya aliyekuwa winga wa timu hiyo, Mfaransa Dominique Rocheteau kustaafu kucheza soka. Pauleta alicheza michezo 211 na kufanikiwa kufunga mabao 109 akiitumikia PSG kabla ya kustaafu. Safari ya kudhihirisha kuwa yeye ni miongoni mwa wapachikaji bora wa mabao ilianza katika timu ya Bordeaux ambapo alikuwa hodari na akafunga mabao 91 katika michezo 130.

Pauleta aliweka rekodi mbili ambazo bado hazijasahaulika baada ya kufunga bao la ushindi kwenye mchezo wa fainali wa Kombe la Ufaransa 2004, ambapo alifunga bao moja katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Chateauroux.

Katika mashindano mengine ya mwisho ya kombe la Coupe de la Ligue, Pauleta alifungua bao la kwanza katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Lens.

3. Kylian Mbappe, mabao 132

Ni jambo la kushangaza kumuona kijana mdogo akiwa kwenye orodha ya wachezaji waliofunga mabao mengi PSG. Kwa sasa Mbappe ana miaka 22 na alijiunga na PSG akitokea Monaco kwa ada ya Pauni 166 milioni, lakini miaka mitatu baadaye imeonekana kuwa biashara nzuri.

Mbappe amecheza michezo 172 na kupachika mabao 132 na wakati wote huo alifanikiwa kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu 2018, 2019 na 2020. Huyu ndiye anaonekana kuwa na rekodi ambazo zitakuwa kikwazo kikubwa kwa Messi kwa sababu hadi sasa amefunga mabao mengi akiwa katika umri mdogo. Ingawa mkataba wake utamalizika Juni, 2022 na inaelezwa kuwa hana mpango wa kuongeza wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.


2. Zlatan Ibrahimovic, mabao 156

Unaanzia wapi kuupinga ubora wa Zlatan Ibrahimovic kutokana na kiwango alichokionyesha katika klabu mbalimbali barani Ulaya. Unapaswa kutoa heshima kwa uwezo wake wa kufunga mabao na ndio maana yupo kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa PSG. Jamaa alikaa misimu minne PSG na kufunga mabao 156 katika michezo 180, na baadaye akatimkia Manchester United.

Licha ya Ibrahimovic kuonekana kuwa mchezaji mwenye kiburi, lakini anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wenye huruma. Jamaa alikuwa tayari kujishusha kwa kina ili kuwaunganisha wachezaji wenzake ndani ya PSG. Ibrahimovic alikuwa mfano wa kuigwa kwa wachezaji wachanga. Katika misimu minne aliyodumu PSG alitwaa kiatu cha ufungaji bora mara tatu. Hii pia ni miongoni mwa rekodi Messi atakayokutana nayo.


1.Edinson Cavani, mabao 200

Tuzo ya mfungaji bora wa muda wote inakwenda kwa Edinson Cavani ambaye aliondoka zake PSG akiwa huru kwenda Manchester United. Cavani alifanikiwa kufunga mabao 200 katika michezo 301 aliyocheza PSG. Mashabiki wa PSG walikwaruzana na uongozi wa timu hiyo baada ya kushindwa kumbakisha mshambuliaji huyo ambaye aliifungia timu hiyo mabao mengi katika miaka saba.

Supastaa huyu alijiunga na PSG akitokea Napoli 2013, lakini msimu wa 2016/17 ndio ulikuwa bora kwa Cavani ambapo alifunga mabao 49 kwenye mashindano yote. Rekodi yake itachukua muda kuvunjwa na ndio kubwa ambayo Messi atakuwa anaifikiria.