Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mcheza Taekwondo wa Tanzania aondoka na matumaini ya ubingwa katika mashindano ya dunia Korea Kusini

Muktasari:

  • Omary mwenye uzito wa kilogramu  54 ataungana  na wachezaji  wengine 140 kutoka nchi 70 duniani kushiriki mashindano hayo ya  Taekwondo.
  • Omary amesema maandalizi aliyofanya  yanatosha kujiamini na kuwa na uhakika wa kushinda.

Arusha. Mchezaji wa Taekwondo, Athuman Omary  ameondoka nchini  leo kuelekea Korea Kusini kushiriki mashindano ya dunia’ World Taekwondo Championship’ yanayotarajiwa kuanza Juni 23 hadi Juni 30.

Omary mwenye uzito wa kilogramu  54 ataungana  na wachezaji  wengine 140 kutoka nchi 70 duniani kushiriki mashindano hayo ya  Taekwondo.

Omary amesema maandalizi aliyofanya  yanatosha kujiamini na kuwa na uhakika wa kushinda.

“Tunawaomba wadau na serikali wajitokeze kutuunga mkono kwani mchezo huu una vijana wenye uwezo mkubwa, lakini bado hatujapata nguvu zaidi katika udhamini,”alisema

Makamu wa Rais wa shirikisho la Taekwondo Tanzania (TTF), Joseph Chuwa alisema maandalizi kuelekea michuano hiyo yamekamilika wanaamani  mchezaji huyo ataiwakilisha nchi vyema.

“Ni mara ya kwanza kushiriki na tuna matarajio ya ushindi kwani kijana wetu amepata mazoezi ya kutosha na muda, tumefuatilia mbinu mbalimbali katika mishuano ya dunia na olimpiki iliyopita tumejiridhisha tutafanya vizuri pia kwa uzito alionao lazima tufanye vyema,”alisema  Chuwa.

Ofisa michezo na Utamaduni jiji la Arusha, Benson Maneno alisema  wanashirikiana na shirikisho la Taekwondo katika kuhakikisha  mchezo huu unapiga hatua jijini hapa .

“Tunamshukuru katibu mkuu wa baraza la michezo Tanzania (BMT) kutoa kibali kinacho waruhusu  kocha na mchezaji kwenda kushiriki mashindano ya dunia,” alisema Maneno.