Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yabanwa ugenini

Muktasari:

  • Hii ni mara ya pili mfululizo kwa United kushindwa kupata alama zote tatu kwenye Ligi Kuu England baada ya kutoka kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Wolves katika mchezo uliopita.

Manchester United imelazimishwa sare kwa mara ya pili mfululizo wakati safari hii ikiwa ugenini dhidi ya Leeds United baada ya timu zote kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Elland Road imeshuhudiwa kipindi cha kwanza timu zote kwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo zikiwa zimetoshana nguvu baada ya dakika 45 za kwanza kumalizika kwa suluhu.

Kipindi cha pili, wenyeji Leeds walianza kwa kasi kwa kufanya majaribio kadhaa kwenye lango la United ambapo mpaka ilipofikia dakika ya 62 ilishuhudiwa Brenden Aaronson akiandika bao la kwanza kwa Leeds baada ya kumalizia pasi ya Pascal Struijk.

Hata hivyo, Leeds haikuchukua muda mrefu kwenye uongozi baada ya Matheus Cunha kuisawazishia United zikiwa zimepita dakika tatu baada ya Leeds kupata bao.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa United kushindwa kupata alama zote tatu kwenye Ligi Kuu England baada ya kutoka kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Wolves katika mchezo uliopita.

Matokeo ya mchezo wa leo yanawafanya Mashetani Wekundu kupanda nafasi moja kwenye msimamo wa ligi kwani imesogea kutoka nafasi ya sita mpaka ya tano ikifikisha alama 31 ambapo itaendelea kusalia hapo iwapo Chelsea itapoteza dhidi ya Man City katika mchezo utakaoanza hapo baadaye kwenye dimba la Etihad.

Kwa upande wa Leeds bado wana wakati mgumu wa kuhakikisha wanapata pointi katika michezo inayofuata ili kukwepa kushuka daraja kwani wamesalia katika nafasi ya 16 wakiwa na pointi 22.