Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Premier League ni leo tena

Muktasari:

  • Kuhusu kuondoka kwa Maresca, kocha wa Man City, Pep Guardiola, alisema Chelsea imepoteza mtu wa maana, huku Mtaliano huyo akihusishwa na mpango wa kwenda kurithi mikoba Etihad.

Manchester, England. Balaa hilo. Chelsea itakayokuwa bila ya huduma ya kocha wake mkuu, Enzo Maresca itakuwa na kasheshe zito huko Etihad itakapokwenda kukabiliana na Manchester City kwenye mchakamchaka wa Ligi Kuu England, Jumapili.

Katika mechi hiyo, kwenye benchi la ufundi la Chelsea kutakuwa na sura mpya, Calum McFarlane, ambaye atakuwa kocha wa muda wa timu hiyo, huku akiwa hana uzoefu wowote wa kuwahi kuongoza kwenye mechi yenye ushindani mkubwa kama hiyo.

Rekodi zinaonyesha kwamba katika mechi tano za mwisho zilizokutanisha Man City na Chelsea, miamba hiyo ya Etihad imeshinda mara tatu na sare mbili, hiyo ina maana, The Blues haijashinda mechi yoyote.

Hata hivyo, kwenye rekodi za jumla, Man City na Chelsea zimekutana mara 56 kwenye Ligi Kuu England, ambapo mechi tisa ni sare, huku Man City ikishinda 20, mara 12 nyumbani na nane ugenini, wakati Chelsea ilishinda 27, mara 14 nyumbani na 13 ugenini. Kazi ipo.

Kuhusu kuondoka kwa Maresca, kocha wa Man City, Pep Guardiola, alisema Chelsea imepoteza mtu wa maana, huku Mtaliano huyo akihusishwa na mpango wa kwenda kurithi mikoba Etihad, hata hivyo leo mashabiki wa Arsenal watakuwa wakiomba Chelsea ishinde ili waendelee gepu la pointi dhidi ya Man City baada ya sasa kuwa imewaacha kwa pointi saba baada ya ushindi wa jana wa mabao 3-2 dhidi ya Burnemouth.

Jumapili hii, kwenye Ligi Kuu England kuna mechi nyingi za kibabe, ambapo Manchester United itakuwa ugenini kukabiliana na mahasimu wao wa jadi, Leeds United, huku Everton ikiwa na kazi ya kuulizana maswali magumu na Brentford.

Kipute kingine kutakuwa baina ya Fulham na Liverpool huku Newcastle United ikiwa na kasheshe zito la kupepetana na Crystal Palace wakati Tottenham Hotspur ikiwa na shughuli mbele ya Sunderland. Mambo ni moto. Kwenye mzunguko wa pili, kila timu inajaribu kusaka pointi mbili ili kujiweka pazuri katika mbio muhimu, ikiwamo ubingwa, Top Four na vita ya kugoma kushuka daraja. Mambo yatakuwaje? Ngoja tuone.