Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rice aibeba Arsenal kileleni

Muktasari:

  • Ni aina ya kina cha kikosi ambacho kwa miaka mingi kilikuwa kinajivunia Manchester City chini ya Pep Guardiola, huku ndoto za Arsenal zikikatizwa na majeraha. Safari hii, mambo yanaonekana tofauti.

Katika mchezo uliokuwa mgumu na wenye presha, Arsenal ilionyesha dalili za kuyumba baada ya beki Gabriel kufanya kosa lililowapa Bournemouth bao la mapema. Hata hivyo, Declan Rice alijitokeza kama shujaa, akifunga mabao mawili ya kwanza ya Ligi Kuu katika maisha yake ya Arsenal, na kuwapa Gunners ushindi muhimu wa mabao 3-2.

Baada ya Gabriel kujirekebisha kwa kufunga bao la kusawazisha, Rice alitumia miguu yake ya kulia mara mbili ndani ya dakika 17 za kipindi cha pili, akipachika mipira miwili wavuni kwa utulivu wa hali ya juu.

Bao lake la pili, alilolimalizia kwa kuibusu kamera, liliwapa Arsenal pumzi kabla ya Bournemouth kupunguza tofauti kupitia kwa Junior Kroupi aliyeingia kipindi cha pili.

Bournemouth walishambulia kwa nguvu hadi dakika za mwisho, wakilalamikia filimbi ya mwisho ya mwamuzi Chris Kavanagh waliyoiona imekatiza mashambulizi yao, lakini Arsenal waliondoka na ushindi huo muhimu.

Rice, aliyekosa mechi dhidi ya Aston Villa kutokana na matatizo ya goti, mejiweka katika orodha ya wafungaji bora wa klabu hiyo msimu huu, akizidiwa na Leandro Trossard na Viktor Gyokeres pekee.

Kocha Mikel Arteta amewahi kumtaja Rice kuwa mmoja wa viungo bora duniani kauli ambayo ni vigumu kuipinga kutokana na mwendelezo wake.

Safari ya Bournemouth si nyepesi tena kama ilivyokuwa zamani. Timu hiyo iliwafunga Arsenal mara mbili msimu uliopita na ilikuwa miongoni mwa wapinzani waliowasumbua The Gunners mapema msimu huu.

Lakini kwa timu inayowania ubingwa, hasa ikiwa inafukuzwa na Manchester City, ushindi dhidi ya timu kama hizi ni lazima.

Baada ya City kujikwaa Sunderland, Arsenal walipata nafasi ya kujitanua kileleni. Ushindi huu umewapa pengo la pointi sita kileleni, huku wakionekana kujifunza kutokana na makosa ya misimu iliyopita ambapo waliongoza ligi katikati ya msimu lakini wakashindwa kutwaa ubingwa.

Kwa muda mrefu katika mchezo huu, Arsenal walionekana kuwa na presha hiyo akilini pasi zisizo sahihi, makosa ya kujilinda na kocha Arteta akiwa mkali zaidi pembeni mwa uwanja. Lakini tofauti safari hii ni uimara wa kikosi.

Kosa la Gabriel lilikuwa kumbukumbu ya makosa ya mabeki wao uwanjani hapo msimu uliopita, lakini beki huyo alijifuta machozi haraka kwa kufunga bao la kusawazisha baada ya jitihada nzuri ya Gabriel Martinelli na Noni Madueke.

Arsenal sasa wana anasa ya kubadilisha wachezaji bila kushusha ubora, hata katika mbio kali za ubingwa. Arteta anaweza kuwapa mapumziko Bukayo Saka na Trossard, akijua ana Martinelli na Madueke waliothibitisha uwezo wao.

Bao la kwanza la Rice lilitokana na pasi ya Martin Odegaard, aliyeanza kurejea katika kiwango chake bora, huku bao la pili likitokana na jitihada za Saka aliyochangia pasi ya mwisho.

Ni aina ya kina cha kikosi ambacho kwa miaka mingi kilikuwa kinajivunia Manchester City chini ya Pep Guardiola, huku ndoto za Arsenal zikikatizwa na majeraha. Safari hii, mambo yanaonekana tofauti.