Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United kumaliza ziara Asia

Muktasari:

  • Mashabiki wa soka barani Asia, hasa Hong Kong, wameupokea ujio wa Manchester United kwa shangwe kubwa, wakijitokeza kwa wingi katika mazoezi ya timu hiyo.

Hong Kong. Kikosi cha Manchester United kinatarajiwa kushuka dimbani leo kuvaana na timu ya taifa ya Hong Kong ikiwa ni mchezo wa mwisho wa ziara yao barani Asia ambako kuna mashabiki wao wengi zaidi duniani.

Kwa mujibu wa takwimu, karibu robo tatu ya mashabiki wa Manchester United wanapatikana barani Asia, hali inayoifanya ziara yao kuwa ya kimkakati zaidi kwa upande wa biashara na uhusiano na wafuasi wao.

Mchezo wa leo utachezwa kwenye Uwanja wa taifa wa Hong Kong saa 9:00 alasiri ambapo United itawakosa baadhi ya nyota wake wa kikosi cha kwanza ambao ni Andre Onana, Diogo Dalot na Harry Maguire.

Katika ziara hiyo, huu ni mchezo wa pili kwa Man United kwani mara ya kwanza walicheza Mei 28 ambapo walikubali kipigo cha bao 1-0 walichokipata dhidi ya kikosi cha ASIAN ALL STARS, huko Kuala Lumpur, Malaysia.

Huu utakuwa ni mchezo wa mwisho katika ziara hiyo ambapo kocha Ruben Amorim ameelezea kuwa anatamani timu yake iondoke na ushindi katika mechi hiyo ili kurudisha fadhira kwa mashabiki wao ambao wameonekana kuja kwa wingi kuiangalia timu yao.

“Nadhani kila mtu anaelewa kwamba huu ni wakati mgumu sana kwa sababu ya msimu tuliokuwa nao na ni vigumu kwa wakati huu kukutana na mashabiki kote duniani. Tunataka kumaliza msimu huu, lakini wakati huo huo tunataka kuwapa mashabiki kitu fulani.

“Jambo muhimu kwa sasa ni kuwapatia furaha mashabiki wetu hata katika wakati mgumu kama huu,” amesema Amorim.

Mashabiki wa soka barani Asia, hasa Hong Kong, wameupokea ujio wa Manchester United kwa shangwe kubwa, wakijitokeza kwa wingi katika mazoezi ya timu hiyo hata wakati wa walipowasili  uwanja wa ndege.