Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majina yatakayoteka usajili Ulaya

Muktasari:

  • Kutokana na hilo, hizi hapa dili 20 zenye nafasi kubwa za kwenda kufanyika kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi litakalohusisha timu za Ligi Kuu England

London, England. Dirisha la uhamisho wa wachezaji la majira ya kiangazi limebakiza siku chache tu kufunguliwa na mashabiki wa soka watakwenda kushuhudia dili za kibabe sana zikifanyika kwenye Ligi Kuu England.

Klabu kubwa kwenye ligi hiyo tayari zimeshatangaza mapema kwamba zitakwenda kufanya usajili mkubwa wakati dirisha litakapofunguliwa, kitu ambacho kitashuhudia wachezaji mastaa wakipishana njiani kubadili timu watakazozitumikia kwa msimu ujao.

Kutokana na hilo, hizi hapa dili 20 zenye nafasi kubwa za kwenda kufanyika kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi litakalohusisha timu za Ligi Kuu England.


Florian Wirtz, Pauni 125 milioni

Manchester City imejiandoa kwenye vita ya kumsajili kiungo huyo mchezeshaji wa Bayer Leverkusen, Florian Wirtz, ambaye mwanzoni waliamini ni mrithi sahihi wa Kevin De Bruyne. Bayern Munich naye iliyoonekana kumhitaji imejiweka pembeni jambo linalofanya Liverpool kuwa pekee wanaohitaji saini yake.


Alexander Isak, Pauni 120 milioni

Arsenal imeweka ubaoni jina la Alexander Isak kwenye orodha ya washambuliaji inayowasaka kwa ajili ya kunasa saini yao kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi. Newcastle United inaweza kuweka ngumu, lakini itawalazimu kupambana kwani Liverpool nao wanaweza kupiga hodi kumtaka straika huyo.


Hugo Ekitike, Pauni 84 milioni

Liverpool, Arsenal, Manchester United, Chelsea na Newcastle United zote kwa nyakati tofauti zimekuwa zikihusishwa na mpango wa kumsajili straika wa Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike, huku West Ham United, Crystal Palace na Everton nazo zikimtaka. Kutokana na hilo, kuna dalili kubwa Ekitike akatua England.


Benjamin Sesko, Pauni 84 milioni

Arsenal imeweka wazi inahitaji saini ya straika kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi na kwenda hilo ndio maana ipo sokoni kumsajili straika wa RB Leipzig, Benjamin Sesko. Arsenal imemweka Sesko kwenye rada zake endapo kama itashindwa kumnasa Viktor Gyokeres kutoka Sporting Lisbon.


Rodrygo, Pauni 80 milioni

Huu unaweza kuwa usajili wa bei nafuu kumpata mkali wa Real Madrid, Rodrygo kwa kiasi hicho cha pesa. Klabu za Ligi Kuu England, Manchester City, Arsenal na Chelsea zimekuwa zikihusishwa na mpango wa kuhitaji huduma yake na sasa kinachosubiriwa ni kocha mpya wa Los Blancos kama ataruhusu.


Rafael Leao, Pauni 70 milioni

Chelsea imemweka Rafael Leao kwenye rada yao ya wachezaji inaowahitaji kuwanasa kwenye kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi ili akakipige England. Arsenal imejiweka pembeni licha ya mwanzoni kuhusishwa naye ikijiuliza kama anaweza kwenda kufiti kwenye timu yao.


Jarrad Branthwaite, Pauni 70 milioni

Manchester United imekuwa ikimpigia hesabu Jarrad Branthwaite kwa muda mrefu na baada ya kuona msimu wao umekuwa hovyo timu hiyo inaweza kupambana kunasa saini ya beki huyo wa kati, ambaye pia anasakwa na Chelsea na Liverpool. Everton itakuwa kwenye wakati mgumu kumzuia asiondoke.


Victor Osimhen, Pauni 69 milioni

Kinachoelezwa ni kwamba Manchester United imeingia kwenye majadiliano kwa ajili ya kusajili straika wa Napoli, Victor Osimhen, ambaye kwa msimu huu alikuwa akipiga kwa mkopo huko Galatasaray na kufanya vizuri. Chelsea nayo inahitaji saini ya staa huyo, ambaye ugumu unaweza kuwa kwenye mshahara wake.


Eberechi Eze, Pauni 68 milioni

Staa wa Crystal Palace, Eberechi Eze amekuwa akizivutia klabu za Manchester City, Arsenal, Newcastle, Chelsea na Tottenham Hotspur na huenda zikaingia kwenye vita kali ya kuwania saini yake kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi. Bila shaka Eze atahitaji kucheza kwenye michuano ya Ulaya.


Matheus Cunha, Pauni 62.5 milioni

Manchester United imeripotiwa kuwa kwenye hatua za mwisho kabisa kukamilisha uhamisho wa Pauni 62.5 milioni kunasa huduma ya mshambuliaji wa Wolverhampton Wanderers, Matheus Cunha, ambaye ameweka wazi anataka kwenda kucheza soka lake Old Trafford hata kama hawachezi michuano ya Ulaya msimu ujao.


Viktor Gyokeres, Pauni 62 milioni

Arsenal imekuwa ikipewa nafasi kubwa ya kunasa saini ya straika wa Sporting, Gyokeres, lakini kwenye usajili huo unaweza kuwaingiza kwenye vita kali na Man United, ambayo inaweza kutumia ushawishi wa pesa na kocha Ruben Amorim ili kumchukua mkali huyo wa kutoka ligi ya Ureno.


Morgan Gibbs-White, Pauni 60 milioni

Manchester City imekuwa ikipambana na kuweka nguvu kwenye usajili wa kiungo wa Nottingham Forest, Morgan Gibbs-White ikihitaji saini yake baada ya kujiondoa kwenye mpango wa kumnasa Wirtz. Kiwango bora cha mchezaji huyo kinampa nafasi ya kwenda kukipiga Etihad chini ya Pep Guardiola.


Xavi Simons, Pauni 60 milioni

Xavi Simons bado tupo kwenye umri ambao anaweza kutumika na makocha kucheza nafasi yoyote ndani ya uwanja. Na kwa timu za Ligi Kuu England ambazo zimekuwa na tatizo la wachezaji wabunifu ndani ya uwanja basi inapaswa kwenda kumchukua Simons na ndiyo maana Man City ipo mstari wa mbele.


Wachezaji wengine

Orodha hiyo ya mastaa 20 ambao wanaweza kubadili timu zao kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi ndani ya Ligi Kuu England ni pamoja na Tijjani Reijnders, ambaye bei yake ni Pauni 59 milioni, huku Man City ikihiatji saini yake. Mshambuliaji Bryan Mbeumo naye yupo kwenye orodha hiyo, bei yake ikitajwa kuwa ni Pauni 55 milioni huku timu zinazomfukuzia ni Arsenal, Newcastle na Man United.

Kiungo Martin Zubimendi, anayetajwa kuwa na thamani ya Pauni 50 milioni, huduma yake inasakwa kwa nguvu zote huko Arsenal na bila shaka msimu ujao anaweza kuwapo kwenye Ligi Kuu England, kama ambavyo anavyofukuziwa Nico Williams wa Athletic Bilbao, anayetajwa kuuzwa Pauni 50 milioni na klabu za Liverpool, Chelsea na Arsenal zikihitaji aende kukipiga Ligi Kuu England.

Beki wa kati Marc Guehi yupo kwenye rada ya Chelsea huku bei yake ikiwa ni Pauni 50 milioni, wakati Milos Kerkez, anayetajwa kuwa na thamani ya Pauni 45 milioni sawa na Jamie Gittens, wakisakwa pia na timu za Ligi Kuu England ikiwamo Man City, Liverpool, Chelsea, Arsenal na Tottenham.