Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bruno yupo tayari kuondoka Man United

Manchester, England. Nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes amesema yupo tayari kuondoka endapo kama mabosi wa klabu hiyo wataamua kumpiga bei kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Fernandes, 30, alishuhudia matumaini ya Man United kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kupoteza mchezo wa fainali ya Europa League mbele ya Tottenham, ambao walifanikiwa kushinda ubingwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 17.

Kiungo huyo mchezeshaji alikuwa mchezaji aliyeonyesha kiwango bora kwenye kikosi cha Man United kilichokuwa na msimu mbaya kwenye Ligi Kuu England msimu huu, lakini ilishindwa kutamba pia uwanjani San Mames kwenye kipigo hicho cha 1-0 kutoka kwa Spurs.

Na Mreno huyo sasa amefunguka kwamba yupo tayari kuondoka Old Trafford kama klabu itaamua kumuuza ili kupata pesa za usajili wa kuboresha kikosi cha kocha, Ruben Amorim. Hata hivyo, kiungo huyo wa zamani wa Sporting Lisbon hajafuta malengo yake ya kuendelea kubaki kwenye kikosi cha Man United ili kukirudisha kwenye ubora wake.

Fernandes amesema: "Siku zote nimekuwa mkweli. Siku zote nimekuwa nikisema nitaendelea kubaki hapa hadi hapo klabu itakapoamua niondoke. Bado nataka kufanya zaidi, kuirudisha klabu hii kwenye siku zake bora. Ila siku klabu itadhani inatosha na muda wa kuondoka umefika, klabu kama hii huwezi kujua. Nimekuwa nikisema na maneno yangu yatabaki kuwa yalivyo. Kama klabu itataka niondoke kwa sababu ya kutaka pesa, basi itakuwa sawa kwa sababu soka wakati mwingine lipo hivyo."

Kauli hiyo imekuja baada ya kuwapo na ripoti za klabu ya Al-Hilal kuwa na mpango wa kuvunja rekodi ya uhamisho ya Uingereza kwa kumsajili Fernandes kwenye dilisha lijalo la uhamisho.

Miamba hiyo ya Saudi Arabia ipo tayari kulipa zaidi ya Pauni 115 milioni, ambayo inaweka rekodi kwenye Ligi Kuu England kwa sasa baada ya Chelsea kulipa kiasi hicho huko Brighton kumsajili kiungo Moises Caicedo mwaka 2023.